MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme
Habari

Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

NAibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle Msukari na Wenzake wa Shule ya Msingi Sun Rise iliyopo Wilayani Kinondoni Dar es Salaam kupelekwa katika Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kujifunza zaidi kwa Vitendo namna mradi huo unavyozalisha Umeme.

Dkt Biteko amesema hayo leo kwa njia ya simu baada ya Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga kutembelea shule hiyo kwa lengo la kumpongeza mwanafunzi huyo ambaye video yake ilijizolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii ambayo Mirabelle alielezea kwa ufanisi juu ya miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa nchini ukiwemo mradi wa Julius Nyerere.

‘’Sisi tukupongeze na tumefurahi kwa umri wako unafuatilia masuala ya Nishati, sasa tutakupeleka kuliona Bwawa la Julius Nyerere uone Umeme unavyozalishwa ili uendelee kujifunza zaidi. Sisi tunatamani kukuona ukifanikiwa zaidi,” amesema Biteko

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema Miradi hiyo ya kimkakati ambayo inatekelezwa nchini ni jitihada za Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha dhamira ya dhati kuendeleza miradi ya umeme nchini ukiwemo mradi wa JNHPP ambao kwa sasa umefikia asilimia 99.8.

“Wakati Mheshimiwa Rais anaingia madarakani, Mradi wa Julius Nyerere ulikuwa asilimia 33, leo tunavyozungumza umefikia zaidi ya asilimia 99 na mashine nane tayari zimeingizwa kwenye gridi ya Taifa. Imebaki mashine moja pekee ambapo mradi uko mbioni kukamilika,” amesisitiza Kapinga

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa wateja Irene Gowelle akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) , amesema wamepokea kwa vitendo agizo la Dkt. Biteko la kuhakikisha mwanafunzi huyo anafanya ziara katika Mradi wa Julius Nyerere ambapo pia amefafanua kuwa elimu na taarifa zinazotolewa na TANESCO zinawafikia walengwa kwa usahihi.

“Hatua hii inatupa nafasi ya kuona kwamba elimu na taarifa mbalimbali tunazozitoa zinawafikia moja kwa moja makundi mbalimbali i?wakiwemo watoto na ndio maana mmeweza kuona Mirabelle akizungumza kwa ufasaha..Sisi kama Shirika la Umeme tutaendelea kufanya hivyo” amefafanua Gowele.

Mwanafunzi huyo licha ya pongezi ,amepewa zawadi mbalimbali ikiwemo Komputa Mpakato (Laptop) pamoja na fedha kiasi cha Sh Milioni Mbili.

You Might Also Like

Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Jengo La TUGHE Wafanyika

Rais Samia kufungua kikao kazi cha watendaji serikalini

TPHPA Yaelezea Vipaumbele Vyake

Wafanyakazi waitwa kupeleka changamoto za kikazi CMA

Muswada wa Kuwalinda Wafanyakazi wa Ndani Waja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Atoa Maelekezo Kwa Chuo Cha Hombolo Kuwajengea Uwezo Viongozi Wa Mitaa Na Vijiji -Kapinga
Next Article Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?