MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara
Habari

Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Wizara ya Maji inaendelea na mpango wa ufungaji wa dira za maji za malipo kabla ya matumizi kwa wateja binafsi, taasisi na biashara, hatua inayolenga kumaliza kero ya ubambikizaji wa ankara za maji kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 28, 2026, kuhusu utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika siku 100 za uongozi wake baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,
Habari Picha 10947
Waziri Aweso amesema changamoto ya malalamiko ya ankara za maji imekuwa kubwa, hivyo wizara imechukua mikakati ya kuboresha huduma kwa wateja wapya mijini na vijijini.
Amesema hadi sasa wizara imenunua dira za maji za malipo kabla 2,271 ambazo zinaendelea kufungwa katika maeneo mbalimbali nchini, akisisitiza kuwa maunganisho ya maji kwa mteja mpya hayapaswi kuzidi siku saba.
Aidha, ameitaka sekta ya maji kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika maeneo yote ya utoaji huduma.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amesema ujenzi wa mabwawa ya ukubwa wa kati ya Gidahababieg, Mwambazi na Mwamashindike unaendelea kwa kasi, yakitarajiwa kuhifadhi zaidi ya mita za ujazo 1,457,000 za maji na kunufaisha wananchi zaidi ya 1,817,800 pamoja na mifugo 356,400.
Habari Picha 10948
Pia amesema serikali imeimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kupanda miti zaidi ya 705,300, kugawa pikipiki 216 kwa Jumuiya za Watoa Huduma za Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs), kulipa Sh. Bilioni 198.84 kwa wakandarasi, kuchimba visima 151 na kulipa fidia kwa wananchi waliopisha miradi ya maji.
Hatua hizo, amesema, zinaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha huduma ya maji safi, salama na endelevu kwa wananchi.

You Might Also Like

Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu

Mgombea Urais SAU Aahidi Kuongoza Nchi Kwa Hofu Ya Mungu

Jisajilini mapema mpate mbolea ya ruzuku

Kasi Ya Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji Yaanza-Kapinga

Rais Samia Awasili Mwanza Kilele Cha Mbio za Mwenge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Sekta Ya Madini Yazidi Kupaa,  Mchango Wake Kwa Pato La Taifa Waongezeka 
Next Article TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?