Na Lucy Lyatuu
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa mfanyakazi wa ndani aitwaye Clemensia Cosmas Mirembe (19) akiwa amejificha kwenye “pagala” maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni.
Mfanyakazi huyo anadaiwa kukimbia baada ya kufanya tukio baya la kikatili la kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali maeneo
ya shingoni mtoto Malick Hashim (6) anayeishi eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda hiyo,Jumanne Muliro upelelezi wa
tukio hilo la kikatili ulianza mara moja na Julia 21 2024 saa 4:00
usiku .
Amesema Julai 17 l, 2024 Jeshi Hilo lilitoa taarifa kuhusu dada wa kazi kufanya tukio baya la kikatili la kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni mtoto Malick Hashim (6) anayeishi eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni.
Amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia.
Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo
kwa hatua zaidi za kisheria.
Amesema Jeshi la Polisi linatoka wito kuwa pamoja na jitihada ambazo zinaendelea za kuzuia vitendo vya kihalifu linawashauri wazazi, walezi, walimu, na jamii kwa ujumla kuwafundisha watoto kujenga tabia ya kutembea katika makuni.
Pia wasikubali kuwakaribu na watu wasiowafahamu, watoto wasitumwe maeneo ambayo kwa mazingira ni hatarishi ikiwa ni pamoja na kuacha kuwatuma watoto wadogo maeneo mbalimbali nyakati za usiku.
Amesema usalama katika jiji la Dar es Salaam umeimarishwa kwenye maeneo mbalimbali na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kushirikiana na vyombo vya dola na wananchi kwa ujumla ili kundeleza jitihada zake za kuzuia vitendo vya kihalifu.