MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi
Habari

CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Walimu Walalamikia Changamoto za Maslahi
Na Lucy Ngowi
DODOMA: CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimeiomba Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, kurekebisha sheria, kanuni na kuweka miongozo itakayohakikisha uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi unakuwa katika mazingira ya usawa na ushindani wa haki unaozingatia utoaji wa huduma bora.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CWT, Joseph Misalaba, mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, katika Kikao cha Baraza la Taifa la CWT kilichofanyika jijini Dodoma.
Habari Picha 11149
Misalaba amesema utekelezaji wa shughuli za vyama vya wafanyakazi nchini umekuwa ukikabiliwa na changamoto zinazotokana na mkanganyiko wa sheria, kanuni na miongozo, hali inayosababisha mazingira yasiyo sawa.
Ametolea mfano uhuru wa upangaji wa ada za wanachama, uliosababisha tofauti kubwa za ada kati ya chama kimoja na kingine.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria, chama chenye wanachama wengi hubeba majukumu ya kuwawakilisha watumishi wote wa kada husika, hivyo kubeba gharama kubwa za uendeshaji, ajira, utetezi na majukumu mengine ya kisheria.
Habari Picha 11150
Hali hiyo ni tofauti na vyama visivyo na wajibu huo, jambo linaloviwezesha kutoza ada ndogo na kuwachanganya watumishi kuchagua vyama kwa misingi ya makato nafuu badala ya huduma.
Pia ameeleza changamoto ya ushughulikiaji wa madeni yasiyo ya mishahara kwa walimu, ambayo hutofautiana kati ya halmashauri, na kusababisha kukosekana kwa usawa.
Ameashauri kurejeshwa kwa kamati za uhakiki na madeni hayo kubebwa na serikali kuu.
Aidha, Misalaba amesema walimu wanaojiendeleza kielimu hawatambuliwi ipasavyo wanaporejea kazini, hali inayowakatisha tamaa.
Ameomba serikali kutafakari upya ili walimu wanaoongeza ujuzi watambuliwe na kupandishwa vyeo stahiki.
Habari Picha 11148
Kwa upande wake, Waziri Deus Sangu amesema serikali imeimarisha majadiliano na CWT, ambapo mwaka 2024/2025 vikao 23 vya ndani na kimoja cha kitaifa vilifanyika.
Ameongeza kuwa walimu 415,719 wamepandishwa madaraja na walimu 110,038 wamelipwa madeni ya mishahara yenye thamani ya takribani Sh Bilioni 125.16, hatua inayoonesha dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu.

You Might Also Like

Muhogo, viazi kuongezewa tija kwenye uzalishaji

UTT AMIS Yazindua kampeni ya ‘Kijiwe Mchongo

Wahamasika Kutumia Mbegu Bora Za Karanga Zilizofanyiwa Utafiti Na TARI

Kafulila: Deni La Taifa Ni Himilivu

PIC Uwekezaji Bidhaa Za Ngozi Utaongeza Mapato

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021
Next Article Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Makamu wa Rais Azindua Mpango wa Kukuza Ujuzi, Ajira kwa Vijana
Habari February 9, 2026
Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri
Habari February 9, 2026
Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021
Habari February 8, 2026
TALGWU Yaipongeza Timu Ya Makatibu Wa Mikoa Na Mawakili Wa Kanda Kwa Kutoa Huduma Bora Kwa Wanachama
Habari February 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?