Na Mwandishi Weti
DAR ES SALAAM; MGOMBEA urais wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, amesema endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Tanzania atahakikisha anaboresha miundombinu ya masoko ya bidhaa za vyakula katika Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na kujenga masoko ya kisasa ili kuwawezesha wafanyabiashara kukuza mitaji yao kupitia biashara wanazozitekeleza.
Mwalim, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Msasani jijini Dar es Salaam wakati akiomba kura kwa wananchi wakichague chama hicho, huku akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe (CHAUMMA), Doricas Fransis, amesema hali ya masoko haiendani na hadhi ya jiji.

Amesema ili kuleta maendeleo ya kimageuzi na kimkakati, serikali ya CHAUMMA itajenga masoko ya kisasa na kuwawezesha wafanyabiashara ruzuku ili wakuze mitaji yao na kuongeza mapato ya nchi.