MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Chatanda: Rais Ametuletea Kiongozi Bora Atakayetusaidia Kutekeleza Ilani Ya CCM
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Chatanda: Rais Ametuletea Kiongozi Bora Atakayetusaidia Kutekeleza Ilani Ya CCM
Habari

Chatanda: Rais Ametuletea Kiongozi Bora Atakayetusaidia Kutekeleza Ilani Ya CCM

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE mteule wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, amesema kuwa Rais amemleta kiongozi bora atakayetimiza vyema majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Chitanda amezungumza hayo muda mfupi baada ya Bunge kuthibitisha jina la Waziri Mkuu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan Kulipendekeza.
Amezungumza hayo leo Novemba 13, 2025 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Amesema tangu kiongozi huyo, Nchemba alipoteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, miradi mingi ya maendeleo nchini imefanikiwa kutokana na usimamizi wake mzuri wa fedha na juhudi za kuongeza mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Amesema kwa msingi huo,  miradi ya maendeleo imekuwa ikitekelezwa katika kila wilaya nchini.
Pia Chatanda ameeleza kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake waliogombea na kushinda majimbo mbalimbali.
Amesema kampeni za UWT ziliwahamasisha wanawake wengi kugombea, matokeo yake wanawake wamefanikiwa kushinda takriban majimbo 37, huku wengine 114 wakipata nafasi za Viti Maalum.
Amesema wanawake hao wanatarajiwa kuwasilisha bungeni changamoto zinazowakabili wanawake nchini, hususan katika masuala ya kiuchumi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri inayotakiwa kutolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatolewa ipasavyo ili kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Chatanda pia amekumbusha ahadi ya Rais Samia ya kutenga Sh. Bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo.
Amesema UWT itahamasisha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo ndani ya siku 100 za utekelezaji wa mpango huo, kama alivyoelekeza Rais.

You Might Also Like

Rais Samia Aweka Jiwe La Msingi Kongani Ya Kwala

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama

JKCI Imeona Wagonjwa Zaidi ya Laki Saba Kwa Miaka Minne

Wanafunzi UDSM, MUM Kushiriki Fainali Ya Kimataifa Mashindano Ya Chinese Brigde

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jackline Mzindakaya: Uteuzi wa Mwigulu Ni Chaguo Sahihi kwa Taifa
Next Article Kigae: Mwigulu Waziri Mkuu Mahiri
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?