MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: CCCC Yaandaa Tamasha La Dragon Boat
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > CCCC Yaandaa Tamasha La Dragon Boat
Habari

CCCC Yaandaa Tamasha La Dragon Boat

Author
By Author
Share
4 Min Read

– Yajivunia Kuwa Sehemu Ya Ujenzi Wa Miundombinu DART

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) Tawi la Tanzania, inajivunia kuwa sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara ya Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART ) inayoendelea katika Mkoa wa Dar es salaam.

Naibu Meneja Mkuu wa CCCC Tawi la Tanzania, Wang Yangkur amesema hayo, wakati akizungumza kwenye Tamasha la Dragon Boat lililoandaliwa na Kampuni hiyo ambayo ni Sikukuu ya jadi ya Wachina inayoadhimishwa Mei kila mwaka kumuenzi Mwanasiasa na Mshairi nchini humo, Qu Yuan.

Amesema kwa miaka mingi wameshiriki katika kujenga miundombinu nchini Tanzania ikiwemo madaraja, Barabara jambo ambalo limeweza kuimarisha urafiki baina ya nchi hizo .

“Kwa miaka mingi na kwa mikono na hekima zetu tumeshiriki katika kujenga miundombinu kote Tanzania, kila daraja na kila barabara inayojengwa siyo tu kwamba inaunganisha miji na vijiji bali pia, inaimarisha urafiki baina yetu,” amesema Yangkur.

Kuhusu tamasha hilo amesema limekuwa likihusisha shughuli mbalimbali za kiutamaduni ikiwemo kutengeneza mpira wa mchele uliofunikwa kwa majani ya mianzi .

“Tamasha la Dragon Boat ni heshima kwa Mshairi mzalendo Qu Yuan na hubeba matumaini ya watu ya baraka, amani na ustawi,” amesema

Pia amesema tamasha hilo linaonesha Historia wakati wananchi wanamsaka kiongozi huyo walirusha mipira ya mchele uliofunikwa kwa majani ya mianzi kwenye mto wakiamini kwamba samaki wangekula mchele huo badala ya kumdhuru Qu Yuan.

Kwa upande wake Meneja anayesimamia masuala ya usafiri na upagaji wa maeneo kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka kutoka Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Muston Mwakyoma ambaye ni miongoni mwa wadau wa Kampuni hiyo.

Amesema wamekuwa wakishirikiama na wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya CCCC katika kuhakikisha miundombinu ya Barabara inakamilika ili kuwezesha mabasi kupita na kusafirisha watu.

“DART tumesanifu miundombinu katika awamu sita awamu ya kwanza ni barabara ya Morogoro ,awamu ya pili imekamilika ambayo ni ya mbangala ya tatu Gongolamboto kuelekea mjini ya nne ni barabara ya Ali Hassan mwinyi na Bagamoyo huku ya tano ikiwa ni Mandela.

Amesema Wakandarasi waliopewa kujenga miundombinu hiyo ni pamoja na Kampuni CCCC ambayo inajenga miundombinu ya awamu nne .

“Kama DART tunaishuru Kampuni CCCC kwa sababu inafanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kuonesha matokeo mazuri na ndio maana leo tupo hapa”amesema

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kawe Kata ya Mzimuni Laira Nassoro amesema wamekuwa wakishirikiana vizuri na Kampuni hiyo katika nyakati zote zenye chagamoto ndani ya mtaa .

Amesema Kampuni hiyo imekuwa ikijitoa na kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya Barabara katika mtaa huo.

Pia amesema Kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika Shule ikiwemo kuwapatia mahitaji maalumu.

“Tumekuwa tukishirikiana kwa ukaribu sana na Kampuni hii tofauti na kampuni nyingine ambazo zimekuwa katika mtaa wetu..Sio mara ya kwanza au ya pili kupitia mashirikiano mazuri tumejumuika nao katika tamasha hili “amesema

Aidha ametoa wito kwa makampumi ya kigeni yaliopo yanayofanya kazi nchini kutokudharau Ofisi za Serikali za mtaa kwani ndio chanzo cha kutoa vibali vyote vinavyohitajika.

You Might Also Like

Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo

TFS Yawataka Wananchi Kufuga Nyuki Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira

Stamico Yapewa Tuzo Na FDH Kujali Wenye Ulemavu

Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa

Biteko Amwakilisha Rais Samia Harambee Ujenzi Kanisa Katoliki

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ununuzi Wa Ndege Anga Za Kilimo Uanze Sasa-Bashe
Next Article Mama Mchumgaji TAG Zinga, Asheherekea Siku Ya Kuzaliwa Na Watoto Yatima, Mazingira Magumu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ushiriki Wa Tanzania Jukwaa La Dunia Waongeza Fursa Za Kimataifa Kukabiliana Na Maafa-Dk Yonaz
Habari June 3, 2025
Shinyanga Kunufaika Na Miradi Ya REA,Wauziwa Mitungi 13,000 Kwa Ruzuku
Habari June 2, 2025
SUA Chatumia Ngamia Mafunzo Ya Vitendo Kwa Wanafunzi
Habari June 2, 2025
Mama Mchumgaji TAG Zinga, Asheherekea Siku Ya Kuzaliwa Na Watoto Yatima, Mazingira Magumu
Habari June 2, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?