MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BRT Kuimarisha Uhusiano Tanzania, China
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BRT Kuimarisha Uhusiano Tanzania, China
Habari

BRT Kuimarisha Uhusiano Tanzania, China

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MRADI wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT), umekuwa ni sehemu muhimu ya urafiki wa  China na Tanzania, wenye kutoa mchango mkubwa katika uchumi, maendeleo na uboreshaji wa maisha.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Usalama Tawi la Tanzania, kutoka Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC), Li Yuling wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya Jiao Zhu China -Tanzania.
Amesema mradi huo wa BRT, awamu ya nne sehemu ya tatu ni sehemu muhimu ya urafiki wa  China na Tanzania, na kwamba sio tu unaboresha usafiri wa umma wa Dar es Salaam ambao ni mji mkuu wa Tanzania, lakini pia unatoa mchango mkubwa katika uchumi.
 “Mradi huo unajumuisha ujenzi wa vituo muhimu vya usafiri, vituo vya mabasi na vifaa vingine vya trafiki. Unalenga kuboresha ufanisi wa usafiri wa mijini, kupunguza msongamano na kuimarisha hali ya usafiri ya wakazi wa eneo hilo,” amesema.
Amesema wameita waandishi wa habari kuonyesha watanzania juu ya dhamira ya makampuni ya Kichina katika maendeleo ya miundombinu inayoyafanya.
“Ili kuendeleza mafanikio hayo na kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, kampuni ya ujenzi ya China tawi la Tanzania imekutana na waandishi wa habari, kuzungumzia mafanikio hayo,” amesema.
Mwakilishi wa Mkandarasi katika mradi huo, You Xudong amesema mradi huo unaoendelea katika eneo la Kivukoni, utachukua miezi 18.
Amesema wanajenga jengo la ulinzi, choo, jengo la tiketi namba moja na jengo la tiketi namba mbili.
Naye Alvin Rujweka, Mwalimu kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT), amesema wamekuwepo na wanafunzi wao wanaosomea uhandisi kwa ajili ya masomo ya vitendo katika kampuni hiyo ya kichina ya CCCC.
Amesema anafundisha ujenzi wa kutumia matofali, mawe na ufundi bomba.
“Wanafunzi wanaoandaliwa kuwa wahandisi, wanapewa elimu ya vitabu na vitendo.  Njia nyingine tunawapeleka kwenye miradi mbalimbali inayoendelea nchini, tunawaunganisha na soko kupitia fani walizosomea, ” amesema.
Mhitimu wa Diploma  DIT mwaka huu 2024, Benson Mbilinyi amesema amepata nafasi ya kujiunga na kampuni hiyo ya CCCC, anafanya kazi kama msaidizi wa mhandisi.
Amesema ametumia elimu yake ya chuo akichanganya na uzoefu wa vitendo anaoupata katika kampuni hiyo.
Ameshauri wanafunzi kujitokeza kwenye fursa kwani yeye mara ya kwanza alikutana na kampuni hiyo ilipokwenda chuoni kwao kuonyesha utendaji kazi kwa vitendo,

You Might Also Like

VETA Mtwara Yawafundisha Wanafunzi Uongezaji Thamani Kwenye Korosho, Mwani

Mawaziri Tanzania Profesa Mkenda, Silaa Mkutanoni Rwanda

Wananchi Watakiwa Kufahamu Sheria Na Miongozo

Wananchi Washauriwa Kujiunga Na Chuo Cha Ualimu Na Ufundi Stadi Morogoro

 Rais Samia aipongeza REA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa
Next Article TALGWU Chafanya Kikao Cha Baraza La Wafanyakazi Dodoma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?