Na Lucy Ngowi
MOROGORO: BARAZA la Wafanyakazi la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), lina jukumu la kipekee la kuchangia katika kuweka mazingira bora ya kazi yenye kuongeza tija, ushirikiano na maendeleo ya wafanyakazi, ambayo ndio uti wa mgongo wa mafanikio ya Taasisi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, mkoani Morogoro.
Nyaisa pia amewakumbusha Wajumbe wa baraza hilo kutekeleza majukumu yao ili kuleta tija na ufanisi mahali pa kazi.
“Tunapokutana hapa ni fursa ya kutafakari mafanikio, kujadili changamoto na kuweka mikakati ya pamoja kwa mustakabali wa Taasisi yetu,” amesema.

Amesema baraza hilo litakuwa na jukumu la kuishauri wakala kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya watumishi, utekelezaji wa mipango na makisio ya mapato na matumizi ya wakala.
Pia kupokea taarifa ya utekelezaji wa wakala na kutoa ushauri, kudumisha ushirikiano kati ya watumishi na wakala katika uendeshaji wa wakala na kushauri kuhusu ustawi wa wakala na maendeleo ya watumishi.
“Pamoja na uzinduzi baraza hili litafanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Taasisi kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kuangalia malengo yaliyopangwa, utekelezaji wa majukumu, changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji, mikakati ya kukabiliana na changamoto husika.
“Vile vile baraza litajadili na kupitisha makadirio ya Bajeti ya Wakala kwa mwaka wa fedha 2025/2026,” amesema.
Wakati huo huo, baraza lilifanya uchaguzi ambapo Ofisa Leseni Mwandamizi Peter Riwa, alichaguliwa kuwa Katibu na Ofisa Usaijili Gift Wazingwa, alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.

Ufunguzi na uchaguzi ulishuhudiwa na.viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Brendan Maro pamoja na Dkt. Hussein
Mugyabuso, pia Ofisa kutoka Ofisi ya
Mugyabuso, pia Ofisa kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Christina Matage,