Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 6 Agosti 2024, alipofungua kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto, Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Mwinyi amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua ya kuimarisha miundombinu ya ZBS kwa kujenga kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto ambacho amekifungua.
Kwa upande mwingine Rais Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kufanya juhudi na kuchukua hatua za kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kwa kujenga miundombinu imara kuwezesha shughuli za kusimamia ubora ziwe za kisasa kwa kuwapatia majengo ya maabara na vifaa vya kisasa.
Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!