MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MAGU – MWANZA: MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, ameahidi kuwa iwapo wataingia madarakani, serikali yake itavunja bodi zote za mazao zilizopo na kuanzisha mamlaka moja itakayoshughulikia mazao ya kimkakati nchini.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilayani Magu, Mwalim amesema mamlaka hiyo mpya itakuwa na jukumu la kuwalinda wakulima na kuinua thamani ya mazao yao, hususan zao la pamba.
Habari Picha 9400
Amebainisha kuwa pamoja na mamlaka hiyo, serikali yake itaanzisha mfuko wa fidia kwa ajili ya wakulima wa pamba ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakumba.
“Leo hii mazao ya biashara yana bodi, lakini zinafanya nini? Wanalipana mishahara na posho, lakini hazimnufaishi mkulima,” amesema Mwalim na kuongeza Serikali inapaswa kuwahudumia wakulima kupitia mamlaka yake ili heshima irudi.
Ameahidi  kusimamia ujenzi wa kiwanda cha kuchambua pamba mkoani Mwanza ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuinua kipato cha wakulima.
Akimkumbuka Mzee Paul Bomani, Mwalim amesema: “Mzee Bomani aliifanya Mwanza iwe na neema ya zao la pamba na alilinda thamani yake kwa uhodari.”
Mwalim aliwataka wananchi wa Magu kumchagua  na chama chake Oktoba 29 mwaka huu, 2025.
Amesisitiza kuwa wakati umefika kwa wananchi kuwa na chama kinachotetea maslahi ya wakulima. “Utajiri wenu ni kero kwao kwa sababu Mungu aliwapa pamba iwainue. Je, leo mtaelekea wapi?” amehoji.

You Might Also Like

BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha

Mipango Zaidi Msiba Wa Cleopa Msuya Kutolewa Na Serikali

Afrika yatakiwa kutokuwa na Matabaka katika kutekeleza AFCFTA 

Ridhiwani Aongoza Majadiliano Ya Taarifa Ya Utekelezaji Wa Majukumu PSSSF

Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Next Article Profesa Laizer Kupambana Na Umaskini, Ujinga, Maradhi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Habari October 28, 2025
Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Habari October 27, 2025
Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Habari October 25, 2025
Shibuda: WanaMaswa jitokezeni kupiga kura bila woga
Habari October 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?