MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge
Habari

Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
KIGOMA:  MKUU wa Wilaya ya Kasulu, Isaac Mwakisu, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao, kwa kuwa matukio hayo ni ya kitaifa, yanaakisi mshikamano wa Watanzania.
Mwakisu amesema hayo leo Jumamosi Septemba Sita, mwaka 2025, wakati wa bonanza la michezo mbalimbali lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiganamo.
Habari Picha 9262
Amesema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa wilayani humo kwa siku mbili, Septemba 17 hadi 18, 2025.
Amesema mwenge huo utapokelewa  katika eneo la Mvugwe, Kasulu Vijijini, kabla ya kuingia Kasulu Mjini siku inayofuata.
“Maudhui makuu ya bonanza hili ni kuwakumbusha wananchi kuwa Mwenge utakimbizwa katika wilaya yetu.
Habari Picha 9263
“Ni muhimu tushiriki kwa wingi ili kuonesha mshikamano wetu na kuthamini amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema Mwakisu.
Pia amesema Mwenge  ni alama adhimu ya taifa, na mapokezi yake ni kielelezo cha uzalendo na dhamira ya kudumisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.
Habari Picha 9264
Amewakumbusha  wananchi kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 29, 2025.
Amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo muhimu kwa kusikiliza sera za wagombea na kuwachagua viongozi wanaowakilisha matarajio yao.
Habari Picha 9265
Katika mahojiano na Mwandishi wa Habari hii,  mmoja wa wananchi Nelstella Kihoza, amesema umati mkubwa ulioshiriki bonanza hilo ni ishara ya mwamko wa kisiasa na uzalendo miongoni mwa wananchi wa Kasulu.
Amesema ni imani pia wananchi watajitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu na Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Habari Picha 9266
Naye Mwalimu Yusufu Hamisi amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa ubunifu wa kuandaa bonanza hilo, akisema limewapa ari mpya ya kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu matukio hayo muhimu ya kitaifa.

You Might Also Like

Mongela Ajiridhisha Ushindi wa Kishindo , Uchaguzi Serikali za Mitaa,Uchaguzi Mkuu CCM

Wahitimu 3,561 wa Mafunzo Ya Huduma Za Afya Ngazi Ya Jamii,Wapatiwa Vitendea Kazi

Mpango Asema Tanzania, Korea Kubadilishana Wafanyakazi

VETA Kujenga Mahusiano Na Wenye Ujuzi, Wabunifu

Waziri Ridhiwani: Vyama Vya Wafanyakazi, Nguzo Ya Mahusiano Mema Mahali Pa Kazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa
Next Article Profesa Kitila Ataja Sababu Za Watanzania  Kumchagua Dkt Samia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?