Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amemshukuru Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na chama kwa ujumla kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kukitumikia chama hicho katika nafasi ya Katibu Mkuu.

Uteuzi huo umeweka historia mpya ndani ya CCM kwani kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwake, chama hicho kimepata mwanamke kushika nafasi hiyo ya juu ya utendaji
Aidha Dkt. Migiro amemshukuru mtangulizi wake, Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kwa kuweka msingi imara atakaoutumia kama njia ya kupita katika kutekeleza majukumu yake.

Ameahidi kushirikiana na wazee wa chama na wafanyakazi wote katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo.
