MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni
Habari

Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
WIDON Matayo, aliyekuwa diwani wa Kata ya Iseke, Manyoni, amedai kunyanyaswa na kudhalilishwa na baadhi ya wagombea wenzake ndani ya CCM wakati wa mchakato wa kura za maoni.
Matayo amewataja Dkt. Pius Chaya, mgombea ubunge wa Manyoni, na Joshua Nzwile, mgombea udiwani kata ya Iseke, kuwa walimkebehi kwa misingi ya ulemavu, wakisisitiza kuwa “kata hiyo haiwezi kuongozwa na mlemavu”, kwa kuwa ni sehemu alikozaliwa Dkt. Chaya.
“Walinidhalilisha waziwazi, wakisema ulemavu wangu ni mkosi kwa kata hiyo,” amesema Matayo, akieleza kuwa alikosa haki sawa ya kushiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani.
Katika hatua nyingine, usiku wa kuamkia Agosti tatu, 2025  Enock Lisasi, mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Wilaya ya Manyoni kutoka tawi la Isimbangulu, alikamatwa nyumbani kwa Nzwile akiwa na orodha ya majina ya wajumbe wapatao 200 na Shilingi 90,000, sehemu ya zaidi ya milioni 15 alizodaiwa kutumia kuhonga wajumbe kwa niaba ya Dkt. Chaya na Nzwile.
Matayo anadai kuwa Lisasi alipobanwa alikiri kutumwa na wagombea hao wawili. Tukio hilo lilithibitishwa na msimamizi wa kura za maoni kata ya Iseke, Barnaba Mushi, ambaye alisema Lisasi alikabidhiwa kwa polisi wa kituo cha Manyoni.
Hata hivyo, Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambqna ba Rushwa (TAKUKURU), mkoa wa Singida, Sosthenes Kibwengo, amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Lisasi kwa kuwa yupo nje ya mkoa huo kwa sasa.
Alipotafutwa, Dkt. Chaya amejibu kwa ufupi kwamba malalamiko hayo yapo katika mchakato wa chama, hivyo hawezi kuyazungumzia kwa sasa.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni, Maimuna Likunguni, amethibitisha kupokea malalamiko na kusema yanashughulikiwa ndani ya vikao halali vya chama.

You Might Also Like

Wanawake Wang’aa Mchakato Uchaguzi Mkuu 2025

Tanzania, Comoro Zaongeza Ushirikiano wa Lugha

Sekta Ya Madini Yazidi Kuchangia Ukuaji Wa Uchumi – Majaliwa

Posta Yaleta   Usafiri Wa Kitalii Ndani Ya Sabasaba

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan, kuongoza Kamati Kuu Maalum kesho

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TOSCI: Mbegu Bora Ni Ajira, Biashara
Next Article Samia, Nchimbi Kuchukua Fomu Ya Urais Kesho
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mgodi Wa Dhahabu Wa Nyanzaga Kunufaisha Wananchi, Ujenzi Wazidi Kupaa
Habari September 23, 2025
Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?