MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Udiwani Kata Ya Mbabala Kizungumkuti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Udiwani Kata Ya Mbabala Kizungumkuti
Habari

Udiwani Kata Ya Mbabala Kizungumkuti

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
BAADHI ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Mbabala, Jijini Dodoma, wameandamana hadi ofisi za CCM Wilaya wakieleza kutokuwa na imani na Diwani mteule wa kata hiyo, Pascazia Mayala.
Mmoja wa wanachama wa CCM, Donarld Mabala, amesema kuwa hatua ya CCM Wilaya kumrejesha diwani huyo ili agombee tena katika kura za maoni haijatenda haki kwa wanachama, kwani tangu achaguliwe miaka 10 iliyopita, hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika.
“Sisi wanachama wa CCM Kata ya Mbabala hatumtaki diwani ambaye amepitishwa tena kwenye kura za maoni. Tangu awe diwani hajawahi kuleta maendeleo yoyote. Badala yake, amekuwa mtu wa kusababisha migogoro isiyoisha, ikiwa ni pamoja na kuwapora wananchi ardhi yao,” amesema Mabala.
Naye mwanachama mwingine wa CCM, aliyejitambulisha kwa jina la Adela Chiwaligo, amesema diwani huyo amekuwa kikwazo kwa wakazi wa kata hiyo, kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi.
“Sisi wana-CCM wa Kata ya Mbabala hatuna chuki naye kwa sababu ya nafasi au jinsia yake. Tatizo ni kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo wanayostahili.
“Kuna miradi mbalimbali ya maendeleo, kama mradi wa barabara ya mzunguko. Vijana wa hapa ndiyo waliopaswa kupewa ajira, lakini yeye huwachagua vijana anaowataka mwenyewe na kuwabagua watoto wetu,” amesema Adela.
“Jambo jingine ni kwamba, anapohitajika kukutana na wananchi kujadili masuala ya maendeleo, hututisha kwa lugha kali, jambo linalokwamisha maendeleo ya kata hii,” ameongeza.
Kwa upande wake, Pascazia Mayala alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo, amesema hawezi kusema lolote kwa kuwa yeye ni mtoto wa CCM.
“Mimi siwezi kusema chochote kwa sababu mimi ni mtoto wa Chama Cha Mapinduzi, na chama ndicho kilichonipitisha kugombea nafasi ya udiwani. Kwa hiyo, waende wakamuulize aliyeniteua. Nitaendelea kuongoza. Waache wapige kelele, nitawanyoosha,” alisema Mayala.

You Might Also Like

Wakandarasi Miradi wa  TAZA Watakiwa Kukamilisha Kazi kwa Wakati 

Wazazi washauriwa kusomesha watoto useremala

Mtindi wa Korosho, Stafeli Wafanyiwa Utafiti UDSM

SIDO jengeni viwanda 20 Kila mkoa-Jafo

Taasisi Za Umma Zasisitizwa Kuzingatia ubora Wa Mikataba Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article UDSM Yabuni Teknolojia Mpya ya Kuhesabu Samaki Kwa Haraka 
Next Article Tanzania Yazindua Mkakati wa Taifa wa Usimamizi Na Uendelevu wa Mikoko
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
VETA Yatahadharisha Changamoto ya Kuzidisha Uchanganyaji wa Chakula Cha Mifugo
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?