RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha sh bilioni 15 kwenye mradi wa kuzalisha umeme wa Mwenga Hydro Ltd uliopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ilipotembelea na kukagua mradi wa kuzalisha umeme wa Mwenga Hydro Ltd ambao unatumia nguvu ya maporomoko madogo ya maji (small hydro power potential) ya mto na upepo katika kuzalisha umeme.