MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari

MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imewafuata wananchi huko waliko kupitia huduma za kliniki tembezi, njia inayoleta  urahisi wa huduma za afya.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa mifupa kutoka MOI, Tumaini Minja amesema hayo wakati wa  Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema kupitia ushiriki wao kwenye maonesho hayo,  MOI imefanikiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 70 waliojitokeza kupatiwa huduma za uchunguzi na ushauri wa kitaalamu, hasa kwa magonjwa ya mifupa, nyonga, magoti na mgongo.
“Tumekutana na wananchi wengi waliokuwa wakihitaji huduma maalum ambazo kwa kawaida hupatikana Dar es Salaam pekee.
“Kupitia kliniki hii tembezi, tumewafikia wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani kwa urahisi zaidi, na bado tutaendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi lengo ni kuona wa Tanzania wananufaika na huduma za matibabu kwa urahisi na ufanisi,” amesema.
Amesema lengo la taasisi hiyo, ni kuhakikisha huduma bora za afya ya ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu na mifupa zinawafikia Watanzania wote kwa usawa.
 “Tunaendelea kutoa huduma hata baada ya maonesho kumalizika, na tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia na Serikali kwa kutuwezesha kufanya haya kupitia kliniki tembezi inayojumuisha madaktari bingwa mbalimbali,” amesema.
Pia taasisi hiyo inatoa elimu ya afya kwa wananchi ili kusaidia jamii kutambua mapema dalili za maradhi sugu yanayohusiana na mifupa na mgongo, hivyo kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa kuchelewa kutafuta tiba.
Amesema huduma hizo za karibu na wananchi zitakuwa endelevu, wametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa kila timu ya madaktari bingwa inapokuwa katika mikoa yao.

“Tumekutana na wananchi wengi waliokuwa wakihitaji huduma maalum ambazo kwa kawaida hupatikana Dar es Salaam pekee,” amesema.

You Might Also Like

NIT yawapika vijana

Watanzania lindeni Viwanda vya Ndani

MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa

Mawaziri Tanzania Profesa Mkenda, Silaa Mkutanoni Rwanda

Wanawake Pelekeni Batiki Kwenye Soko Huru La Afrika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Next Article Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Benjamin Mkapa Yaanzisha Mfuko Kuchangia Wagonjwa Wa Upandikizaji Figo,Uloto Wasiokuwa Na Uwezo
Habari June 26, 2026
Huduma Ya Kupandikiza Uume Benjamin Mkapa Sh mil 10
Habari June 26, 2026
Waziri Sangu Awataka Waajiri Kutumia Fursa ya Msamaha wa Tozo wa NSSF
Habari June 26, 2026
PPRA Yahimiza Makundi Maalum Kunufaika na Zabuni za Serikali
Habari June 25, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?