Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI sita na Walimu wawili kutoka Chuo Cha Ufundi VETA-Dar es salaam wanatarajiwa kuelekea Jiji la Nagai katika Jimbo la Yamagata, Japani kushiriki katika mpango wa mafunzo kwa vitendo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kundi hilo litashiriki mafunzo ya vitendo wa wiki mbili katika Shule ya Ufundi ya Nagai kuanzia Juni 16 hadi 27 2025 ikiwa ni Mpango wa Kubadilishana katika Elimu ya Ufundi nchini Japani.
Taarifa imeeleza kuwa Mradi huo ni sehemu ya mpango wa majaribio unaolenga kukuza ujuzi na taluma kati ya Tanzania na Japani.
Imeeleza Japani inakabiliana na upungufu mkubwa wa wafanyakazi, naTanzania ikiwa na idadi inayokua ya vijana wenye motisha, mpango huo unalenga kuleta jitihada zenye manufaa kwa pande zote kwa kujenga uwezo wa rasilimaliwatu.
Taarifa imeongeza kuwa mradi unatarajiwa kuchangia katika kutatua matatizo yao husika kama ajira ya vijana nchini Tanzania, pamoja na kuongeza rasilimali watu katika viwanda vya ndani vya Japani kutoka Tanzania.
Imeeleza mpango huo wa kubadilishana pia unafanya kazi kama mpango mkuu wa JICA Afrika Hometown, ambao umejipanga kimkakati na TICAD 9.
Taarifa ilifafanua kuwa mpango huu unatoa mfano wa jinsi ushirikiano wa serikali za mitaa kati ya Japani na mataifa ya Kiafrika unavyoweza kuleta ustawi wa pamoja na uamsho wa kikanda.
Imeeleza kuwa mafunzo ya Kitaalamu kwa Vitendo katika kozi za Mechaniki na Elektroniki.
Kadhalika kupitia program hiyoitawezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa ambavyo havipatikani nchini Tanzania.
Pia amesema wataweza Kujifunza moja kwa moja mbinu za kiufundi za Kijapani, Mafunzo ya utamaduni wa Kijapan, lugha ya Kijapani, kutembelea sehemu za kitamaduni.
Aidha watakuwa na ziara za viwandani katika Jiji la Nagai na mafunzo ya vitendo katika viwanda vya Kijapani.