Na Lucy Lyatuu
KUELEKEA Uchaguzi Mkuu, Katibu Tawala wa mkoa wa Dares Salaam, Dk Toba Nguvila amewataka madereva pikipiki maarufu kama bodaboda na bajaj kujiepusha na vikundi vya watu vinavyotumika vibaya kwa ajili ya kuchafua taswira yay a Tanzania.
Amesema hayo Dares Salaam wakati akizindua ripoti ya utafiti dhidi ya kundi hilo iliyofanywa na Chama Cha Wafanyakazi Wa Mawasiliano Na Usafirishaji Tanzania (COTWU-T) na Shirila La Friedrich Ebert Stiffung(FES) Tanzania.
Akizungumzia uchaguzi amelitaka kundi hilo kutambua kuwa hakuna mbadala wa Tanzania, wala Dar es Salaam nyingine na hakuna mbadala wa mambo mengi yanayofanywa mazuri.
“Ukiona utulivu uliopo ni kwa sababu tumejenga Tanzania nzuri…Tunaye Rais ambaye ana 4R kama kuna jambo lolote ambalo ni gumu yafaa kulizungumza vizuri na kama kuna jambo lolote linalohitaji viongozi, mtuone hata jana,leo na kesho,” amesema Dk Nguvila.
Amesema kutokana na hayo pindi wakiwaona watu wanaotumika vibaya waonywe, waambiewe ukweli, kwa kuwa Rais aliyepo ni shujaa sana.
“Mama ana uwezo mkubwa sana, tuna viongozi wazuri, mawaziri wazuri, watendaji wazuri sana, kama kuna jambo linaloonekana haliendi vizuri tuelezane, tuko tayari,” amesema.
Amesema wanapokwenda kwenye uchaguzi wasiende kutumika bali wakatende matendo memo ya kuleta uzalendo kwa nchi, yenye amani, usikivu na nidhamu kwa taifa, yenye maadili ya kitanzania ya kiakisi upendo, umoja na mshikamano.
“Tuenende kwa ajili ya kutafuta fedha na kujenga uchumi Tanzania ni nchi ya amani, biashara ziko saa 24 ili mfanyekazi mkitafuta fedha,” amesema