MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BRAC Tanzania: Upo Umuhimu Sekta Binafsi, Serikali Kushirikiana
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BRAC Tanzania: Upo Umuhimu Sekta Binafsi, Serikali Kushirikiana
Habari

BRAC Tanzania: Upo Umuhimu Sekta Binafsi, Serikali Kushirikiana

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
TAASISI isiyo ya kiserikali ya BRAC Tanzania, imesema upo umuhimu kwa wadau mbalimbali kutoka  sekta binafsi, kushirikiana na serikali na watunga sera kupunguza umasikini kwenye jamii nchini.
Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi  wa taasisi hiyo, Joydeep  Roy wakati wa kusherehekea miaka 53 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.
Amesema BRAC ni miongoni mwa taasisi zisizo za serikali ambazo zimekuwa zikitenga sehemu ya mapato yake, kurejesha kwa jamii hususani katika mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja,
Ikiwamo katika aneo la makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo, uwezeshaji wa vijana, sekta ya elimu, kilimo, programu ya kuondoa umasikini.
“Na tunafanya  hivyo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii na kuiunga mkono serikali katika kuhudumia jamii ya Watanzania.
“Kwa mfano katika kusherehekea miaka 53 tangu kuanzishwa kwa taasisi yetu, mwaka huu tumejumuika na jamii kwa kutoa vifaa muhimu kwenye sekta ya elimu katika shule ya wasichana ya kulea watoto yatima ya Bethesaida iliyopo Mbezi Mpiji Magohe,”amesema.
Joydeep amesema  taasisi yao itaendelea kujitolea  kusaidia makundi mbalimbali  ili kuhakikisha inakuwa sehemu ya kuongeza thamani kwenye maisha ya Watanzania.
“Mwaka huu tumekusudia kuongeza  jitihada zaidi katika kuwa karibu na jamii katika kukuza umoja na ushirikiano  na tumepanga kuwa na mijadala mbalimbali ya kujenga,
” Tunaamini  mijadala hiyo itatoa fursa ya watu kusema changamoto, uvumbuzi pamoja na mambo hasi na chanya wanayokutana nayo,” amesema.
“Bado tunaamini kwamba tutaendelea kuongeza miradi mingine kwa ajili ya kusaidia jamii yetu kwa sababu sisi sote tunapaswa kuwajibika kuihudumia na si serikali pekee,” amesema.
Mwenyekiti na mwanzilishi  wa Shule ya Sekondari  Bethsadia , Raymond Machary pamoja na kuishukuru BRAC kwa msaada kwao, amesema bado shule hiyo ina uhitaji wa misaada kwa kuwa inachukua wanafunzi  wenye uhitaji ambao wengi wao hawana wazazi.

You Might Also Like

MSD Yaokoa Zaidi Ya Mil. 15

WCF Yatakiwa Kuongeza Nguvu Kusajili Waajiri

Rais Samia Kuzindua Mfuko wa Mikopo Wenye Kianzio Cha Sh. Bilioni 2.3

Sheikh Akemea Wanawake,Wanaume Wanaovaa Vibaya 

Baraza La Madiwani Lampongeza Rais Samia Kwa Utekelezaji Wa Ilani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Miaka Minne Ya Samia, TANESCO Yajivunia Kudhibiti Upotevu Wa Umeme
Next Article USCAF Yawapatia Mafunzo Ya TEHAMA Walimu 1585
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?