Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: ” LEO na mimi nataka kuchangia kidogo umuhimu wa VETA na kwanini uende VETA.
VETA ni muendelezo wa transformation ya masuala ya Ufundi stadi, kwa faida ya GEN-Z ni kwamba awali ilianza National Vocational Training Centre ( NVTC) ikaenda tena kuwa National Vocational Training Division ( NVTD) kabla ya kuwa VETA.
“Binafsi sikusoma kidato cha tano na cha sita, baada ya kumaliza kidato cha nne nikajiunga na NVTC kusomea ufundi Umeme wa majumbani na kupata cheti cha Daraja la III,”.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano cha Shirika la Reli Tanzania (TRC), Fredy Mwanjala ametoa mapni yake hayo ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam( JNICC).
Mwanjala amesema stadi za ujuzi alizopata zilimsaidia kupata kazi za kufunga umeme kwenye nyumba za watu ikiwemo pia maghorofa.
” Niliutumia ujuzi huo kwa kujipatia kipato kabla sija develop interest kuwa journalist. Nikaenda chuo na kufanikiwa kuhitimu shahada mbili za mawasiliano ya Umma.
“Faida niliyonayo sasa ni kwamba hakuna fundi anayeweza kunidanganya kuhusu masuala ya umeme wa majumbani aidha ninaweza pia kumpa ushauri rafiki yangu ama yeyote kuhusu namna bora ya kufunga umeme nyumbani kwake,” amesema.
Akielezea umuhimu wa VETA, amese stadi anazopata mtu zinamsaidia mtu hata akiwa na maarifa ya kitu kingine.
“Mfano halisi mimi ni mtu wa mawasiliano lakini faida niliyopata VETA, ni kwamba hakuna fundi atanidanganya kuhusu Installation kwa mfano wire za 1.5mm na 2.5 mm zina matumizi gani ndani ya nyumba, kwanini Umeme una trip, taa zote iwe za incandescent, ama bulb, holder’s, nafunga mwenyewe, najua ku trace short imetokea wapi na kwa vipi naweza kussolve, najua aina gani ya cable za kutumia kwa matumizi husika.
“Suala la back up sipigwi, najua kujumlisha watts za vifaa vyangu na ninamwambia muuzaji anipatie back up ya watts ninayoitaka kwa matumizi yangu..
“Hiyo ni miongoni mwa faida za kuwa na stadi kutoka VETA,” amesema.
Pia amesema kiuchumi, mtu anaweza kujiajir ama kuajiriwa kutokana na ujuzi. Kwenye ushindani wa ajira, kidato cha nne mwenye stadi ya VETA hawezi kuwa sawa na kidato cha sita ambaye ametoka shule hajapata ujuzi wowote ama Mwenye diploma.
Mwanjala amesema mtu akiajiriwa kwenye taaluma nyingine lakini ana stadi katika eneo la ujenzi anaweza kupata zabuni na akawapa vibarua wafanye kazi huku yeye akisimamia kutokea kazini kwake.
“Lengo langu ni kushea umuhimu wa VETA na faida zake,” amesisitiza.