Na Danson Kaijage
DODOMA: TAASISI za kidini zinazofanya biashara badala ya kutoa huduma zinatakiwa kulipa kodi ya Serikali na si vinginevyo.
Kamishina wa TRA Yusuph Mwenda, amesema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeeo kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma juu ya mafanikio ya Mamaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo baada ya kuulizwa swali na Mwandishi wa Habari wa Mfanyakazi Tanzania, aliyetaka kujua ni utaratibu gani uliowekwa kwa taasisi za dini zinazojenga vitaga uchumi na kuwakodosha wafanya biashara.
Akijibu swali hilo amesema, taratibu zinaonesha wazi kwamba taasisi za dini zinazotoa huduma zinapewa misamaha ya kodi.
“Tunatoa misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa huduma lakini kama taasisi inafanya biashara au imejenga jengo na inakodisha inatakiwa kulipa kodi kwani taasisi hiyo inafanya boashara,” amesema.
Pia amesisitiza watanzania kulipa kodi kwa hiari kwa faida ya maslahi mapana kwa taifa.