MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mazao Bora Ya Kilimo Kutoka Tanzania Yavutia China
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Mazao Bora Ya Kilimo Kutoka Tanzania Yavutia China
Makala

Mazao Bora Ya Kilimo Kutoka Tanzania Yavutia China

Author
By Author
Share
5 Min Read
  • Ni Katika Maonesho Ya Nchi Za Kimataifa Ya Biashara China

Na Waandishi Wetu

MAONESHO ya Saba ya Uingizaji ya Kimataifa ya China yalifunguliwa rasmi Novemba tano, 2024 – Shanghai China.

Katika maonesho hayo China ikiwa mwenyeji, Nchi ya Tanzania iliweza kujizolea umaarufu mkubwa.

Mwalimu wa Lugha ya Kiswahil kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) Ning Yi, katika makala haya anasema kwamba, umaarufu huo wa Tanzania umetokana na faida yake kijiografia na uwepo wa rasilimali nyingi za asili ulichochea umaarufu katika maonesho hayo.

Hivyo ikaimarisha na kuleta nguvu mpya katika ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Tanzania.

Mojawapo ya kivutio ni“Dhahabu Nyeusi” ya Tanzania—Harufu ya Kahawa Yafika Shanghai.

Mwandishi wa makala haya, anasema kahawa ya Tanzania inajulikana duniani kwa ladha yake ya kipekee na utamu wake wa ajabu na inajivunia sifa moja ijulikanayo kama “Dhahabu Nyeusi”.

Kwamba mashamba yaliyopo maeneo ulipo Mlima Kilimanjaro yaliyojaa ardhi ya volkano yenye rutuba hutoa punje bora ya kahawa ambayo yameipa kahawa ya Tanzania sifa ya “Mfalme wa Kahawa ya Afrika”.

Ning anasema katika Maonyesho ya Sita ya Uingizaji ya Kimataifa ya China, kampuni moja ya utengenezaji wa kahawa kutoka Tanzania ilifanikiwa kupata wasambazaji wa kahawa nchini China, na kufungua soko kubwa la China kwa bidhaa zake.

Anasema Mwaka wa 2024, kampuni hiyo imejitokeza tena katika maonyesho na kupeleka bidhaa mpya zaidi.

Kadri soko la kahawa linavyoendelea kupanuka nchini China, mauzo ya kahawa ya Tanzania yanatarajiwa kuongezeka.

Pia Tanzania haikuishia kwenye kahawa pekee, pia kwenye Mwani uliopewa jina la “Dhahabu ya Kijani” Kutoka Zanzibar—Mwani Wakuza Ajira kwa Wanawake wa Zanzibar.

Mwani ni bidhaa maalum inayozalishwa kwa wingi kisiwani Zanzibar, ambayo inaweza kutumika moja kwa moja kama saladi au kama malighafi ya viwanda.

Kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, uzalishaji wa zao la mwani ulikuwa umezidi tani 12,000 kwa mwaka huko Zanzibar.

Ning anasema kwa sababu ya thamani yake ya kipekee ya virutubisho na faida za kimatibabu, mwani unaitwa “Dhahabu ya Kijani” na wakazi wa Zanzibar.

Mwani hautumiki kwenye chakula pekee bali hutumika pia kwenye vipodozi, dawa na vitu  vinginevyo.

Katika Maonesho hayo makubwa, bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na mwani zilikuwepo wakiwemo wafanyabishara wa Tanzania.

Bidhaa hizo zilivutia watu mbalimbali waliofika kwenye maonesho hayo.

Anasema bidhaa hizo hazionyeshi ustadi pekee wa ufundi wa jadi kutoka Zanzibar, lakini pia zilitengeneza fursa nyingi za ajira kwa wanawake wa Zanzibar.

Pia Mazao ya Korosho Yanavyoendelea kuongezwa thamani na kutoa bidhaa mbalimbali.

Nchi ya Tanzania ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa korosho duniani.

Katika miaka ya karibuni, korosho za Tanzania zimepata umaarufu mkubwa kwenye soko la China. Katika Maonyesho yaliyopita korosho za Tanzania zilikuwa moja ya bidhaa maarufu, na kuvutia wanunuzi wengi.

Mnamo mwaka 2021, kampuni moja ya biashara ya kimataifa kutoka Hunan, China, ilifanikiwa kupata uzabuni wa kuingiza korosho za Tanzania, na kuanzisha uhusiano mzuri wa biashara ya korosho kati ya China na Tanzania.

Maonyesho ya 2024 Yasaidia Kuinua Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Tanzania

Ning anasema mnamo mwaka 2023, biashara ya pande mbili kati ya China na Tanzania ilifikia Dola Bilioni 8.78, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka 2022.

China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Tanzania kwa miaka minane mfululizo. Maonyesho ya Uingizaji ya Kimataifa ya China yamekuwa jukwaa bora kwa bidhaa za Tanzania kuingia kwenye soko la China, na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Vilevile anasema Tanzania na China zinafanya juhudi kubwa kupanua ushirikiano kati yao. Tanzania imepanua mauzo ya bidhaa za kilimo kwa China ili kuongeza pato la taifa.

Na kampuni za China zimefanikisha miradi ya reli, madaraja, bandari, mifumo ya huduma za maji na mingineyo nchini Tanzania, ikileta mabadiliko makubwa.

Bidhaa nyingi za kipekee za Tanzania ambazo awali hazikujulikana sana kwa walaji wa China sasa zimepata nafasi katika soko la China kupitia maonyesho ya kimataifa, na kuwa mfano hai wa ushirikiano wa kibiashara unaofaidisha pande zote mbili.

Mwandishi : Zhou Li, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)

Barua pepe: sylvanzhou@foxmail.com

Mwandishi 2: Ning Yi ni mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU)

Barua pepe:02706@shisu.edu.cn

You Might Also Like

Mafanikio Ya Veta Katika Kuadhimisha Miaka 30:

Matukio ya Wafanyakazi Yaliyojiri kuanzia Januari 2024, Hadi Leo Disemba 31, 2024

MATUKIO YA MISIBA KWA WATU MAARUFU YALIYOJIRI KUANZIA JANUARI 2024, HADI DISEMBA 2024

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Usafirishaji Wa Mizigo SGR Mbioni Kuanza
Next Article Asilimia 22 Ya Vijana Wanakumbwa Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukizwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?