Na Danson Kaijage
DODOMA:TAASISI ya Tiba ya Mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) imesema viungo bandia vya binadamu vinauzwa bei kubwa kutokana na malighafi zinazotengeneza viungo hivyo kutozalishwa hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt.
Mpoki Ulisubisya amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma,juu ya mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amefafanua hilo baada ya kuulizwa kwa nini bei ya viungo bandia vya binadamu huuzwa kwa bei ghali ilhali wagonjwa wengi hawana uwezo wa kumudu hiyo gharama.
Amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani ili kupunguza ajali.
Kuhusu waendesha pikipiki amesema kuna haja ya vyombo vinavyosimamia usalama wa barabarani kuwakazia madereva bodaboda kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara na wakati mwingine kuhakikisha dereva ambaye hajapitia mafunzo ya udereva na asiyekuwa na lesini kutotumia chombo cha moto.