MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaongeza Bajeti Mfuko Wa Utamaduni Na Sanaa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaongeza Bajeti Mfuko Wa Utamaduni Na Sanaa
Habari

Serikali Yaongeza Bajeti Mfuko Wa Utamaduni Na Sanaa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: MWAKA wa fedha 2024/25 Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania umepata ongezeko la Sh. Bilioni tatu tofauti na mwaka wa fedha 2023/24 ambapo ulikuwa na bajeti ya Sh. Bilioni1.6.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba, alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utekelezaji na Maendeleo ya mfuko huo kwa muda wa miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akielezea mafanikio hayo amesema, awali bajeti ya mfuko huo ilikuwa chini ya kiwango cha uendeshaji na uboreshaji wa mfuko,suala lililokuwa likipunguza ufanisi wa utendaji.
Pia amesema tangu kupatikana kwa uhuru mfuko huo haujawahi kuwa na bajeti kubwa kama ilivyo sasa.
Kwa maelezo yake, sekta ya utamaduni ilikuwa ikipata ruzuku ya Sh.Milioni 500 ambayo ilikuwa haiwezi kukidhi malengo ya sekta hiyo na baadaye katika mwaka wa fedha 2023/24 iliidhinishwa bajeti ya Sh.  Bilioni 1.6.
Na mwaka wa fedha 2024/25 ikaidhinishwa Sh.Bilioni tatu jambo ambalo halijawahi kutokea katika sekta hiyo.
Amesema kiasi kilichoongezeka ni Sh. Bilioni 1.4 ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 87.5 huku
Serikali ikiongeza chanzo kipya na endelevu cha mapato ya Mfuko kinachotozwa katika vibebeo tupu vya Kazi za Sanaa (Tozo ya Hakimiliki).
Ameeleza kuwa , kupitia chanzo hicho,  Mfuko hupata gawio la asilimia 10 ya mapato yote yanayokusanywa na chanzo hiki kimeanza kutekelezwa Mwezi Septemba, 2023.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mfuko umefanikiwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.2 kwa miradi 359 ya Sanaa iliyozalisha jumla ya ajira 497,213.
Akielezea mchanganuo wa miradi aliyataja maeneo ya miradi iliyowezeshwa ni muziki (miradi 78), filamu (miradi 90), maonesho (miradi 65), Ufundi (miradi 103) na Lugha na Fasihi (23).
Pia ameitaja Mikoa iliyofikiwa ni 18 ambayo ni Dar- Es Salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Geita, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kagera, Mara, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Simiyu, Kigoma na Katavi.

You Might Also Like

Watanzania lindeni Viwanda vya Ndani

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani, Mwenyekiti wa CCM Pwani, wawanadi wagombea wa CCM

Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050

Profesa Mkenda Aitaka TAEC Kusomesha Watumishi

CPC chatambua juhudi za Rais Samia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TIC Yapaa Kiuchumi Afrika
Next Article Kimwaga Mwenyekiti Mpya DCPC, Ahimiza Nidhamu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaweka Mkazo Kufufua Viwanda Musoma Ili Kuongeza Ajira
Habari April 24, 2026
Program Ya Mama Samia Ya Kurasimisha Ujuzi Yazinduliwa
Habari April 23, 2026
TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu
Habari April 23, 2026
Bajeti Yadhihirisha Uhakika Wa Nishati Nchini
Habari April 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?