Na Mwandishi Wetu
DODOMA: JUMUIYA ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) imeiomba Serikali kutoa mikopo ya fedha na vifaa vya uzalishaji wa maudhui katika Tasnia ya habari, kama inavyofanya katika tasnia nyingine.
Mratibu wa Jumuiya hiyo Gilbert Boniface ametoa ombi hilo katika mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini, uliofanyika Februari 13-14, 2025, jijini Dodoma.

Amesema ili kuendeleza na kuimarisha kazi za uandishi na uzalishaji wa maudhui ya ndani katika mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa na msaada wa kifedha na vifaa vya kisasa.
Amesema msaada huo utachochea ubunifu na kuhakikisha vyombo vya habari vinavyotumia mitandao ya kijamii vinakuwa na ufanisi na ubora wa juu katika utoaji wa habari.