MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Msigwa Azikumbusha Taassisi Za Serikali, TANROAD Ikielezea Mafanikio Yake
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Msigwa Azikumbusha Taassisi Za Serikali, TANROAD Ikielezea Mafanikio Yake
Habari

Msigwa Azikumbusha Taassisi Za Serikali, TANROAD Ikielezea Mafanikio Yake

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: WAKUU wa Taasisi za Serikali wametakiwa kutoa taarifa zao za utekelezaji wa shughuli za maaendeleo kwa miaka minne ya uongozi wa  Rais Samia Suluhu Hasani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, ametoa maagizo hayo leo Jumatatu Februari 17, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari Jijini hapa, wakati Wakala  wa Barabara Tanzania (TANROAD), ulipotoa taarifa yake,
Msigwa ambaye pia ni  Msemaji mkuu wa Serikari wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu (TANROAD) Ephatar Mlavi, amesema ni wajibu wa taasisi hizo kuhakikisha zinatoa mawasilisho ya taarifa ya maendeleo kadri walivyopangiwa.
Naye Mkurugenzi huyo wa TANROAD,  Mlavi amesema Serikali imefanikisha kujenga mtandao kwa barabara za lami,madaraja na viwanja vya ndege ambavyo vipo katika hali mzuri.
Amesema Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa kilometa 15,625.55 zimekuwa katika hatua mabalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenye urefu wa kilometa 1,365.87 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na barabara zenye urefu wa kilometa 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
 “Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,052.94 na madaraja mawili  zimefanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina na Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami.
“Vilevile, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 4,734.43 na madaraja kumi unaendelea. Aidha, miradi ya barabara yenye urefu wa takriban kilometa 5,326.90 na miradi saba ya madaraja ipo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kufanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina  ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.
“Katika kipindi tajwa madaraja makubwa tisa yamekamilika kujengwa kwa gharama ya Sh.i Bilioni i 381.301 kama ifuatavyo: Gerezani (Dsm), Daraja jipya la Tanzanite  (Dsm), Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Kiyegeya (Morogoro), Ruaha (Morogoro), Ruhuhu (Ruvuma), Mpwapwa (Dodoma) na daraja la Msingi (Singida). “Amesema Mlavi.
Katika maelezo yake amesema kuwa Madaraja 10 ambayo ni Kigongo  Busisi (Magufuli Bridge – Kilometa 3.0), Lower Mpiji (Meta 140), Mbambe (Meta 81), Simiyu (Meta 150), Pangani (Meta 525), Sukuma (Meta 70), Kerema Maziwani (meta 80), Kibakwe (meta 30), Mirumba (Meta 60) na Jangwani (Meta 390) ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya Sh. Bilioni 985.802.
Amesema jumla ya Madaraja makubwa 19 yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni: Godegode (Dodoma), Ugala (Katavi), Kamshango (Kagera), Bujonde (Mbeya), Bulome (Mbeya), Chakwale (Morogoro), Nguyami (Morogoro), Mkundi (Morogoro), Lower Malagarasi (Kigoma), Mtera (Dodoma), Kyabakoba (Kagera), Mjonga (Morogoro), Doma (Morogoro), Sanga (Songwe), Kalebe (Kagera), Ipyana (Mbeya), Mkondoa (Morogoro), Kilambo (Mtwara) na Chemchem (Singida).
Katika kipindi cha miaka hiyo minne hali ya barabara kuu na zile za mikoa imeendelea kuimarika ambapo barabara zilizo katika hali nzuri na wastani zimekuwa karibu asilimia 90 ya jumla ya mtandao wote wa barabara wenye Kilometa 37,225.72.

You Might Also Like

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

Tanzania,  na Taasisi ya BVGH kuimarisha huduma za saratani

Marekebisho ya sheria huangalia mazingira ya sasa na yajayo – Tume

TPHPA Tuna Mchango Mkubwa Katika Utoshelevu Wa Chakula – Ndunguru

Theluthi mbili ya nguvu kazi ya taifa ipo kwenye kilimo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani Awataka Wananchi Kuboresha Taarifa Zao Tayari Kwa Uchaguzi Mkuu
Next Article JUMIKITA Yaiomba Serikali Mikopo Ya Fedha, Vifaa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?