MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaeleza Mikakati Ya Kuwezesha Vijana Katika Soko La Ajira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaeleza Mikakati Ya Kuwezesha Vijana Katika Soko La Ajira
Habari

Serikali Yaeleza Mikakati Ya Kuwezesha Vijana Katika Soko La Ajira

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: SERIKALI inakabiliana na tatizo la ajira kwa kubuni na kutekeleza programu maalum zinazowawezesha vijana kujifunza kwa vitendo kupitia sekta zinazozalisha ajira kwa wingi.
Sekta hizo ni kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho iliyobora (BBT), ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining for a better Tommorrow (MBT).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo leo Februari 10, 2025 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpendae, Toufiq Turky.
Ridhiwani pia amesema serikali  inafanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Tolea la Mwaka 2023 ambayo yanasisitiza mafunzo kwa kuandaa wataalamu.
“Kupitia ujenzi wa miundombinu ya Kimkakati muhimu inayochochea uchumi, vijana wameajiriwa na kunufaika na urithishwaji ujuzi kutoka kwa wataalamu wa nje mfano ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na barabara za mwendokasi (BRT),” amesema Mhe. Kikwete
Vile vile amesema Serikali itaendelea kubuni na kutekeleza programu ya kukuza ujuzi ambayo inalenga kukuza ujuzi kwa nguvu kazi ili kuwezesha vijana kushindana katika soko la ajira mfano mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi waliopo kazini na kwa wajasiriamali.
Waziri Kikwete amesema mkakati mwingine ni kuweka msisitizo kwenye matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), katika kuzalisha fursa nyingi za ajira kwa vijana.
“Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha vijana wanaandaliwa ili wapate ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na hivyo kumudu ushindani wa ajira,” amesema.
Turky amehoji kuna mpango gani wa kuwandaa vyema vijana waweze kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania ili kukabiliana na upungufu wa ajira nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri Kikwete ametaja mipango ya serikali katika kuwaandaa vijana ili kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

You Might Also Like

Majaliwa Asisitiza Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji

CCM yavunja rekodi – Makala

Huduma ya Mahakama ya Mwanzo yasogezwa Wilaya ya Ubungo

Boti yazama abiria 14 kati ya 21 waokolewa

Rais Samia aungwa mkono na Tughe, watalii 800 watua Ngorongoro

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dendego Achangisha Bilioni 1.7, Ujenzi Ofisi Ya CCM
Next Article Wana Dodoma Wakoshwa Na Uboreshaji Mitaala
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu
Habari July 9, 2025
NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani
Habari July 9, 2025
Katiba Na Sheria Kutoa Kipaumbele Kusikiliza Malalamiko Ya Wananchi
Habari July 9, 2025
Vumbi la Nyuki Lapewa Uzito Singida: Latajwa Tiba ya Asili Yenye Virutubisho 99
Habari July 9, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?