Na Waandishi Wetu
RELI ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ina uhusiano mkubwa baina ya Nchi ya China na Afrika.
Historia ya reli hii inaonyesha kuwa ilijengwa kuanzia mwaka 1970 na kukamilika mwaka 1975.
Ina urefu wa kilomita 1,860.5, inaanzia Dar es Salaam, mji wa bandari nchini Tanzania, kwa upande wa mashariki na kuishia Kapiri Mposhi katikati mwa Zambia kwa upande wa magharibi.
Ujenzi wa reli unalenga kuunganisha mikoa yenye shaba nchini Zambia na bandari moja kwa moja, ili kusaidia Zambia ambayo haikupakana na bahari kujikita kiuchumi bila ya kutegemea Afrika Kusini na Zimbabwe.
Reli hiyo kwa kuwa ni ya miaka mingi imechakaa, Uwezo wake wa uendeshaji umepungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa ajili ya kustawisha tena reli ni lazima kufanyiwa ukarabati wa kisasa.
Ukarabati wake unahusiana na ufanisi wa usafirishaji wa rasilimali za madini, pia unaathiri maendeleo ya bandari nchini Tanzania.
Hivyo Disemba mwaka juzi 2023, timu ya wataalamu wa China ilifika nchini Tanzania, ikafanya ukaguzi wa kina kuhusu uendeshaji na ufundi wa Reli ya TAZARA.
Baada ya utafiti wa kina, Februari mwaka jana 2024, upande wa China uliwasilisha mpango wa kukarabati Reli ya TAZARA na kupanga kuuanzisha mradi huo kwa mfumo wa ushirikiano wa kibinafsi na umma, ili kukamilisha ukarabati wa kisasa wa reli.
Utiaji Saini wa Makubaliano ya Maelewano (MoU) Wafungua Ukurasa Mpya Wakati mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 ulipofanyika, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kwa pamoja walishuhudia hafla ya utiaji saini Makubaliano ya Maelewano (MoU) kuhusu mradi wa kustawisha njia ya Reli ya TAZARA.
Makubaliano hayo yalionyesha mwanzo wa ukarabati na ustawishaji wa Reli ya TAZARA.
Hivyo Kazi ya ukarabati wa Reli ya TAZARA italeta athari kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi ya kieneo.
Lakini habari njema ni kwamba, Makao Makuu ya TAZARA Mkoani Dar es Salaam, yalitoa taarifa kuwa ukarabati huo utakapokamilika uwezo wa usafirishaji wa kila mwaka wa waendeshaji wote kwa wastani utaongezeka kutoka tani 50 hadi tani 200.
Uongezekaji huo wa tani utaongeza nguvu kuu itakayokuza maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania na Zambia.
Hakuna shake kwamba mradi huo utatoa ajira,, ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya viwanda katika maeneo yaliyo karibu.
Hivi sasa upande wa Reli ya TAZARA unafanya mazungumzo kwa hamasa kuhusu makubaliano ya kibali maalumu cha uendeshaji cha miaka 30 pamoja na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya China (CCECC).
Kampuni hiyo inalenga kuanzisha ukarabati wa miundombinu na treni utakaochukua muda wa miaka miwili baada ya makubaliano kutiwa saini.
Eneo la Kumbukumbu ya TAZARA Lafunguliwa kurithi urafiki kati ya China na Afrika
Eneo la Kumbukumbu ya TAZARA lilifunguliwa rasmi katika Wilaya ya Chongwe, mkoani Lusaka, nchini Zambia. Wafanyakazi Wachina 36 waliopoteza maisha yao katika ujenzi wa reli wanazikwa katika eneo hilo.
Jambo hilo linaashiria urafiki na ushirikiano wa kina baina ya China na Zambia.
Katibu mkuu katika Wizara ya Utalii ya Zambia, Evans Muhanga, ameeleza katika hafla ya uzinduzi kwamba eneo hilo la kumbukumbu litawajulisha watu wengi zaidi wa Zambia historia ya ujenzi wa Reli ya TAZARA na kurithi urafiki kati ya China na Afrika.
Mradi wa ufufuaji wa Reli ya TAZARA si marudio ya historia tu, bali pia ni maratajio kwa siku zijazo. Katika muktadha wa enzi mpya ya ushirikiano kati ya China na Afrika.
“Reli hii itafufuliwa na kuwa ukanda unaounganisha mioyo ya watu wa China na Afrika. Kupitia ujenzi wa Mpango wa “Ukanda na Njia” wenye ubora wa juu,
“Tunalenga kukuza maendeleo ya kiuchumi ya kieneo na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika, ili kujenga Jumuiya ya karibu zaidi ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja. Ufufuaji wa Reli ya TAZARA utakuza mawasiliano ya kieneo,
“Pia utatia nguvu mpya katika Afrika na hata ushirikiano baina ya China na Afrika.
“Tunaamini kwa dhati kwamba kupitia juhudi za pamoja, Reli ya TAZARA itakuwa mandhari nzuri Barani Afrika na kushuhudia historia tukufu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika,,”
Waandishi wa Makala hii ni :
Song Yiting Mwanafunzi wa Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU)
yiting_mo@126.,com
Ning Yi Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shangai (SISU)