MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa
Habari

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: SERIKALI imeyapokea na inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo matatu ya marekebisho ya Sheria ya Mazingira sura 191.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais (Muungano na Mazingira) Hamad Masauni amesema hayo na kuyataja mapendekezo hayo ni kanuni ya kulifanya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa Mamlaka,
Pua umuhimu wa kutunga Sheria ya Uchumi wa Buluu na kutambuliwa kisheria kwa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
Masauni amesema hayo wakati akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kwa Mwaka 2024 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Jackson Kiswaga bungeni jijini Dodoma.
Waziri Masauni ameipongeza Kamati hiyo kwa mchango wake na kusema kuwa ni wenye maono katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira.
Amesisitizana kuwa dhamira ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na Kamati hiyo.
“Kama ambavyo tuliwaahidi kwenye kamati, Mheshimiwa Spika naomba mbele yako niahidi tutayafanyia kazi yale yote mliyotushauri wakati wa michango ya wabunge na taarifa ya kamati,
“Tayari tumeandaa mpango kazi kabambe ambao mpaka leo tunavyozungumza hakuna hata kipengele kimoja hatujakitekeleza kama tulivyojipangia kwa hiyo tunakwenda vizuri,” amesema.
Amesema ni matamanio ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuona maeneo hayo matatu yaliyoainishwa ikiwezekana Bunge lijalo kwa ushirikiano mkubwa lipitishe.
Awali, akiwasilisha taarifa hiyo Kiswaga amesema azimio la Bunge kuwa Serikali itoe mafunzo kwa wataalamu wa ndani wawe na ujuzi wa kuandaa mapitio ya tathmini ya athari kwa mazingira limetekelezwa kikamilifu.
Kiswaga ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga amesema Ofisi ya Makamu wa Rais katika kipindi cha Februari hadi Desemba 2024 imetoa mafunzo hayo kwa jumla watumishi 75.

You Might Also Like

Tani 27, 550  za ufuta zenye thamani ya bilioni 80 zimeuzwa

Dendego Achangisha Bilioni 1.7, Ujenzi Ofisi Ya CCM

Mbunge Ndoinyo Asema Imani ya Wananchi kwa Rais Samia Yazidi Kuimarika

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

Miradi Dodoma Yamkuna Rais Samia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wachimbaji Wadogo Wafikiwa
Next Article Ukarabati wa Reli Ya TAZARA Wafungua Ukurasa Mpya China, Afrika
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

DCF Atembelea Banda Wizara Mambo YA Nje, Atoa Pongezi
Habari June 20, 2026
June 20, 2026
Uncategorized June 20, 2026
PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Habari June 20, 2026
Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa
Habari June 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?