Na Mwandishi Wetu
DODOMA:WATUMISHI wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wametakiwa kuongeza uwajibikaji, nidhamu ya kazi, kuboresha utendaji kazi, kuimarisha ushirikiano na viongozi ili kuendelea kudumisha amani, utulivu na usalama wa nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa wito huo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza Kuu la wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma.
“Michango yenu ilenge kutekeleza falsafa ya 4Rs za Mheshimiwa Rais, ambazo ni Maridhiano, Mabadiliko, Ustahimilivu na Kujenga upya” amesema.

Naye Naibu wa Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amewapongeza watumishi kwa kuendelea kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.
Mweyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu amasisitiza watumishi watumie baraza hilo kutoa michango yenye tija itakayowezesha Wizara kutekeleza majukumu ya kila siku.

“Kufanyika kwa Mkutano huu wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Wizara ni fursa kwa watumishi wote kushirikishwa katika kupanga mipango ya Wizara Kupitia majadiliano ya pamoja,” amesema.