Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), pamoja na cha Zambia, vinatarajia kukutana mwanzoni mwa mwaka ujao 2025 kwa ajili ya kujadili ubinafsishwaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Eddo Makata amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa Mfanyakazi Tanzania kuhusu ubinafsishwaji unaoenda kufanyika ambapo serikali za nchi zote mbili zimeshakubaliana.
Makata amesema serikali za nchi hizo mbili zimekubaliana kampuni kutoka China ya CCECC kuendesha reli hiyo.
“Ubinafsishaji huu utaendana na masharti kadhaa kwa sababu wameshasaini MOU, baada ya kusaini wanaingia mkataba sasa katika mkataba wanaoingua sisi kama vyama vya wafanyakazi TRAWU na wenzetu walioko Zambia tutakutana kuona ni kitu gani kimepangwa kwa ajili ya mfanyakazi wa TAZARA.
” Anaondolewa kwenye taasisi au haondolewi. Ni nini anafanyiwa. Kwa hiyo tunategemea mwakani mapema tutapigania maslahi ya mfanyakazi huyu wa TAZARA,” amesema.