Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ameipongeza Mahakama kwa kutoa kipaumbele kwa wenye Ulemavu katika kada zote za kiutendaji.
Ridhiwani ametoa pongezi hizo alipokuwa akifunga mafunzo ya Watumishi wa Serikali, Mahakama na Taasisi za Umma yaliyodhaminiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi Afya mahala pa kazi (OSHA).

Ameitaka mahakama kuendelea na mapambano ya kupinga unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu.
Ameeleza watendaji wa mahakama hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha Haki na Maslahi ya Wenye Ulemavi yanasimamiwa kwa kutunga sera na mipango mbalimbali inayowezesha Sera hizo kutekelezeka.