MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali
Habari

Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu
WATUMISHI wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, ubunifu, juhudi, maarifa na upendo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Dkt. Khatibu Kazungu wakati akifungua Baraza la Tano la Wafanyakazi wa REA leo Disemba7,2024 jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kazungu amewataka watumishi REA kuwahudumia Watanzania kwa maarifa na upendo hususan katika kufikia malengo ya Serikali yanayotarajiwa katika Sekta ya Nishati.

“Niwasisitize wajumbe wa mkutano huu kusikiliza kwa umakini, kufuatilia na kutoa maoni na ushauri utakaokuwa chachu ya kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora ya nishati kwa wananchi,” amesisitiza Dkt. Kazungu.

Aidha, amewaagiza watumishi REA kufanya kazi kwa ubunifu huku wakizingatia maadili ya utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Vile vile, amewataka kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa maadili kama vile rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kazungu ameipongeza REA kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati na kuwaahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaunga mkono kwa manufaa ya umma.

Naye, Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Heri Mkunda ameipongeza Menejimenti ya REA kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyakazi na kusisitiza na kuomba ushirikiano huo uimarishwe ili kuongeza ufanisi na weledi katika kutekeleza majukumu yao.

Awali Mkurugezi Mkuu wa REA, Hassan Saidy ameeleza kuwa uhusiano wa Menejimenti na Wafanyakazi umeimarishwa katika nyanja zote na kuahidi kuendelea kuahirikiana na TUGHE ili kuongeza ufanisi wa wafanyakazi katika utendaji kazi.

You Might Also Like

Simbachawene: Nitaheshimu Mfumo Wa Uongozi Na Kushirikiana

Jeshi la polisi kumhoji anayesambaza taarifa za uongo

Tume Ya Mipango Yaelekeza Waandishi Wa Habari Kutoa Elimu Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050

Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025

Chatanda Ampongeza Samia, Aahidi Kuinua Wanawake Kiuchumi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wanaodaiwa Kumuua Ofisa TRA Washikiliwa na Polisi
Next Article Wamiliki Migodi Wapewa Siku 30 Kufanya Usajili
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?