Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: DAWA inayokabiliana na ugonjwa wa maambukizi ya bakteria kwa njia ya mkojo ( UTI), na fangasi ijulikanayo kama ‘ Lab Spray Disinfectant” imepatikana.
Mwalimu wa Maabara kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA), Ally Issa amesema hayo katika Kongamano na maonyesho ya tisa ya Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu, yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sa
Issa amesema bakteria wengi wa magonjwa hayo hupatikana kwenye vyoo vya umma hivyo, kabla ya kutumia choo dawa hiyo inapulizwa kisha mtumiaji anatumia.
“Kama unasumbuliwa na fangasi kwenye miguu unachukua dawa hii na kuipulizia kwenye eneo lililoathirika. Dawa hii imetengenezwa na Glycerin, Ethanol, Benzoic na Salicylic kwa ajili ya kuua bakretia wa UTI na fangasi,” amesema.
Pamoja na dawa hiyo pia wametengeneza mafuta ya mwarobaini kwa ajili ya kujikinga na kudhibiti mbu.
Issa amesema mafuta hayo yametengenezwa kwa utaratibu maalum kwa kutumia majani ya mwarobaini, mchaichai na mafuta ya nazi.
“Mafuta haya hayana kemikali yoyote kwa sababu yametengenezwa na vitu asili. Ukiyapaka mwilini hakuna mbu atakayekusogelea,” amesema.