Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.
Ridhiwani amesema hayo wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana jijini Dar es Salaam.
Amesema serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo, kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Vijana.

Kwa maelezo ya Ridhiwani tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki, Caroline Mugalla, pamoja na watendaji wengine.