MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BOT Yafungia Applications 69 Za Mikopo Mtandaoni
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BOT Yafungia Applications 69 Za Mikopo Mtandaoni
Habari

BOT Yafungia Applications 69 Za Mikopo Mtandaoni

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT), imefungia Majukwaa na Programu Tumizi 69, zilizokuwa zinajihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali kwa kutokuwa na leseni na idhini ya kufanya biashara hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba imeeleza kuwa majukwaa na programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu Agosti 27, 2024.

Tutuba amesema mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda mlaji wa huduma za fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Ametaja Majukwaa na Programu Tumizi hizo kuwa ni BoBa Cash, Hewa Mkopo, Money Tap, Soko loan, Bolla Kash – Bolla Kash Financial Credit, Hi Cash, Mpaso chap loan – Mkopo kisasa, Sunloan, BongoPesa-Personal Online Loan na HiPesa.

Mengine ni Mum loan, Sunny Loan,Cash Mkopo, Jokate Foundation Imarisha Maisha, My credit, Swift Fund, Cash pesa, KOPAHAPA, Nikopeshe App na TALA.

Pia Cash poa, Kwanza loan, Nufaika Loans, TikCash, CashMama, L-Pesa Microfinance, Okoa Maisha – Mkopofast, Twiga Loan, CashX, Land cash, Pesa M, TZcash, Credit Land, Loanplus, Pesa Rahisi, Umoja, Eaglecash TZ, M-Safi, PesaPlus, Usalama Na Uwakika Mkopo Dk15 na Fast Mkopo.

Vile vile Mkopo Express, PesaX, Ustawi loan, Flower loan, Mkopo Extra, Pocket loan, Viva Mikopo Limited, FUN LOAN, Mkopo haraka, Pop Pesa, VunaPesa, Fundflex, MkopoFasta, Premier loan, Yes Pesa, Get cash, MkopoHaraka, Safe pesa, ZimaCash na Getloan.

Nyingine ni Mkopohuru, SasaMkopo, Getpesa Tanzania, Mkoponafuu, Silk loan, Hakika loan, Mkopowako na Silkda Credit.

“Benki Kuu inautahadharisha Umma kutojihusisha na Majukwaa na Progamu Tumizi hizo ‘’Applications’. Aidha, Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia programu hizi ili kuepusha Umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali vya Mamlaka husika.

“Benki Kuu imechapisha na itaendelea kuhuisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma za mikopo katika tovuti yake,” imesema taarifa hiyo.

 

You Might Also Like

RC Chalamila Ataka Reli Za Ndani Ya Mkoa Kusafirisha Abiria, Kupunguza Msongamano

Wanazuoni Kujadili   Dira  Itakayojenga  Uchumi Unaofikia   Dola Trilioni Moja

Rais Samia Aridhia Malipo Ya Fidia Barabara Ya Afrika Mashariki

Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Wanaotumika Vibaya Waonywe

Tanzania kujiimarisha zaidi kidiplomasia – Majaliwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vyama Vya Wafanyakazi Vihimize Waajiri Kutoa Taarifa WCF, Zinazohusu Wafanyakazi Wanaopata Ajali, Ugonjwa Kazini
Next Article Mkakati Wa Utekelezaji Wa Sera Ya Malikale Lango La Fursa Za Utalii
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?