Na Lucy Ngowi
DODOMA:RAIS Samia Suluhu Hassan amebariki mabadiliko ya sheria itakayotambua hesabu za mapumziko ya mzazi atakayejifungua mtoto njiti.
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), jijini Dodoma.
Ridhiwani amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za sheria hiyo.
“Zamani ilikuwa mzazi akijifungua mtoto njiti suala la mapumziko ni huruma ya mwajiri. Sasa tunaanza kuhesabu siku mtoto aliyezaliwa mpaka miezi tisa, ndipo hapo unaanza kuhesabu miezi ya kawaida,” amesema.