MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: RC Serukamba Aiunga Mkono REAUgawaji Wa Mitungi Ya Gesi Iringa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > RC Serukamba Aiunga Mkono REAUgawaji Wa Mitungi Ya Gesi Iringa
Habari

RC Serukamba Aiunga Mkono REAUgawaji Wa Mitungi Ya Gesi Iringa

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba ameunga mkono juhudi za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) za kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia ipatayo 9,800 mkoani humo itakayoendelea kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Serukamba amezungumza hayo leo Novemba 18, 2024 mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA katika mkoa huo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Advera Mwijage.

Serukamba ameipongeza REA kwa mradi huo na miradi mingine mbalimbali inayoendelea kutekelezwa mkoani humo ikiwemo ya kufikisha umeme kwenye vijiji na vitongoji.

“Nawapongeza REA kwa kuendelea kusambaza mitungi ya gesi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Nawapongeza pia kwa kuendelea kufikisha umeme katika maeneo mbalimbali, natoa rai kwenu kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa katika kutekeleza miradi hiyo nchini ili kuifanya kuwa na tija kwa wananchi.” Amemalizia Serukamba.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Mwijage ameeleza kuwa, mitungi hiyo itasambazwa katika wilaya tatu ikiwemo Kilolo, Iringa na Mufindi ili kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama.

Ameongeza kuwa kampuni ya Lake Gas itaanza kusambaza gesi za kupikia mkoani humo mwezi Januari mwaka 2025 ili wananchi waanze kunufaika na nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Advera amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya ujenzi wa vituo vya mafuta kwa kuwasilisha maombi REA.

“Mradi utahusisha ujenzi wa vituo vya mafuta kuanzia lita 10,000 hadi lita 15,000 za mafuta na naipongeza Serikali kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii, ” Amesema Mwijage.

You Might Also Like

Mawakili Wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Katiba Ya Nchi Wanapoandika Sheria

NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria

Mbarawa Aagiza Matumizi Ya Kitufe Utambuzi Wa Dereva

Tanzania Yatumia Wiki Ya Nishari India Kunadi Vitalu Vya Mafuta Na Gesi Asilia

Awamu Ya Pili Uboreshaji, Uwekaji Wazi Wa Dafatri La Wapiga Kura Kuanza Mei

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kamati Ya Bunge Yaipongeza TVLA Uzalishaji wa chanjo
Next Article Ridhiwani Apongeza Kurudi Kwa Gazeti La Mfanyakazi TANZANIA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card
Habari May 19, 2025
Shen Zhiying: Mkongwe Aliyeanzisha Kozi Ya Kiswahili Nchini China
Makala May 19, 2025
Uongozi CHADEMA Kanda Ya Kati Upo Imara
Habari May 18, 2025
Msisubiri Kupewa Amri, Ufanyaji Usafi Kwenye Maeneo Yenu – Lugendo
Habari May 18, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?