MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo ya Jamii, Yaipongeza Serikali Uwekezaji Kiwanda Cha Chai
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo ya Jamii, Yaipongeza Serikali Uwekezaji Kiwanda Cha Chai
Habari

Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo ya Jamii, Yaipongeza Serikali Uwekezaji Kiwanda Cha Chai

Author
By Author
Share
2 Min Read
Ridhiwani Kikwete Aguswa Na Ajira Pamoja Na Uhakika Wa Soko La Chai Kwa Wakulima
Na Mwandishi Wetu
TANGA: UWEKEZAJI uliofanywa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Wafanyakazi wa Umma (PSSSF), katika Kiwanda cha Chai Mponde, kilichopo Bumbuli Lushoto Tanga, umewezesha ajira kwa wananchi.
Hilo limedhihirika wakati Kamati  ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii,  ilipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuona shughuli zinazofanywa na kamati hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema miongoni mwa faida za kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa wananchi pamoja na uhakika wa soko la chai kwa wakulima.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatma Toufiq amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa  uwekezaji kwenye kiwanda hico cha Chai Mponde.
Ametoa pongezi hizo alipotembelea kiwanda hicho na wajumbe wa kamati kwa lengo  la kuona namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi.
Pia amepongeza mifuko ya WCF na PSSSF  kwa uwekezaji wenye tija wanaoufanya kwenye kiwanda hicho.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa WCF, Dkt. John Mduma amesema kiwanda hicho kitawawezesha wananchi wa Lushoto, Bumbuli Korogwe na maeneo jirani kupata kipato kitakachowainua kiuchumi kwa kuwa wengi wanategemea zao hilo.
Mmoja wa wakulima wa zao hilo, Mwanyemi Mdoe ameishukuru serikali kwa hatua iliyoichukua ya  kufufua kiwanda hicho, ambacho kinasaidia kukuza Uchumi wao.

You Might Also Like

Msisubiri Kupewa Amri, Ufanyaji Usafi Kwenye Maeneo Yenu – Lugendo

Stamico Yapewa Tuzo Na FDH Kujali Wenye Ulemavu

Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya SGR

Serikali Inaendelea Kutekeleza Mradi wa Kupeleka Umeme Grid Ya Mtwara Na Lindi- Kapinga

Serikali Kuendelea Kuboresha Sheria za Ulinzi wa Watoto

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article
Next Article Afrika yatakiwa kutokuwa na Matabaka katika kutekeleza AFCFTA 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bodi ya Maziwa Yatoa Mafunzo ya Ubora, Usalama wa Maziwa Katika Maonyesho ya Nane Nane
Habari August 7, 2025
Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane
Habari August 7, 2025
Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Habari August 7, 2025
Mramba Afungua Mafunzo Ya Teknolojia Ya Nishati Jua Kwa Watalaam
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?