Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 5

Wakumbushwa Kufuata Utaratibu Wa Kuboresha, kurekebisha sheria 

Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WIZARA na Taasisi mbalimbalii zilizopo  nchini zimeagizwa kuitumia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, zinapotaka  kufanya mapitio au utafiti wa Sheria zao.
Kwa kuwa kutofanya hivyo ni kukiuka Sheria na taratibu kwani Tume hiyo imeundwa kwa kazi hiyo.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi ametoa agizo hilo alipokuwa akipokea taarifa nane  za utafiti uliofanywa na Tume hiyo,katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Wizara hiyo.
Profesa Kabudi ametoa agizo hilo kutokana na ombi la Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Winifrada Korosso kueleza kuwa moja ya changamoto inayoikumba Tume hiyo ni baadhi ya Taasisi na Wizara kupeleka mapendekezo ya Sheria pasipo kupitishia kwenye Tume hiyo na kufanyiwa utafiti wa kina.
Akizungumzia hilo, Kabudi ameeleza hasara inayoweza  kuikumba serikali kwa  kupokea mapendekezo yasiyopitia kwenye Tume ya Kurekebisha Sheria kuwa yanasababisha Sheria hizo kutodumu kwa muda mrefu.
” Kwa bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa serikali upo hapa napenda ifahamike kwamba wizara  au Taasisi yeyote inayotaka kufanya maboresho au kutungwa kwa Sheria mpya ni lazima maboresho hayo yafanywe na Tume ya Kurekebisha Sheria kwa kuwa huko ndiko kwenye wabobevu,” amesema.
Amesema sio sawa kwa serikali kushughulikia msaada wa Sheria ambao utadumu kwa muda mfupi na  kuhitaji maboresho,, changamoto hiyo itaondoka endapo kila mmoja atafanya kazi yake.
Kwa upande mwingine ameipongeza tume hiyo  kwa kazi nzuri inayoifanya ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wizara yake
kutekeleza falsafa ya serikali.
Tume ya Kurekebisha Sheria ndio chombo chenye jukumu la kufanya mapitio na utafiti wa Sheria zote hapa nchini  ili kuzifanya ziishi kwa  muda mrefu.
.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.