MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TEA, TotalEnergies Marketing Ltd Wakabidhi Madawati 130 Wilayani Kibiti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TEA, TotalEnergies Marketing Ltd Wakabidhi Madawati 130 Wilayani Kibiti
Habari

TEA, TotalEnergies Marketing Ltd Wakabidhi Madawati 130 Wilayani Kibiti

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya TotalEnergies Marketing Ltd kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wamekabidhi madawati 130 katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani na Shule ya Msingi ya Kitunduza Wilayani Kibiti mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ushirikiano baina yao Katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo aliongoza hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Kolombo Katika hafla hiyo aliagiza madawati hayo yatunzwe vizuri kwa manufaa ya wanafunzi wa shule hiyo, na kuongeza kuwa wamekuwa wakinufaika na miradi mbalimbali ya TEA ikiwemo wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Katika Shule ya Msingi Kitundu.

Naye Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Marketingi Tanzania Ltd, Getrude Mpangile amesema madawati hayo 130 ni sehemu ya madawati 200 yenye thamani ya sh milioni 25.9 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa shule tatu za Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Kutokana na msaada huo Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani imepata madawati 65, Shule ya Msingi Kitundu madawati 65 na Shule ya Msingi Makukburi ya Mkoani Dar es Salaam madawati 70.

Ameelezea matumaini yake kuwa msaada huo utasaidia kuweka hamasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii hivyo kuchangia kukuza ufanisi na ufaulu wa shule zilizonufaika na madawati hayo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi TEA, Mwanahamisi Chambega amekumbusha shule zilizonufaika na msaada huo wa madawati kuyatunza vyema.

 

“Miongoni mwa majukumu ya TEA ni kutafuta rasilimali fedha kutoka kwa wadau mbalimbali na kuzigawa Katika Taasisi za Elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hivyo tunawakumbusha kutunza vifaa hivi,” amesema.

 

 

 

You Might Also Like

Thamani ya Fedha Ionekane Kwenye Utekelezaji wa Miradi-Nyamoga

Tulia Atoa Taarifa Kifo Cha Ndugai

MOI Kuendesha Kambi Maalum Ya Uchunguzi,  Ushauri Wa Kitabibu Kwa Wazee

UDSM Yamtunuku Rais AfDB Shahada Ya Heshima Ya Sayansi

Biteko Amwakilisha Rais Samia Harambee Ujenzi Kanisa Katoliki

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Samia Azindua Shule ya Msingi ya Mchepuko wa Kiingereza Songea
Next Article Usekelege: Kati ya Migogoro Tunayoipokea Ipo ya Wafanyakazi Majumbani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?