MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: OUT yaunda Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini Mradi wa HEET
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > OUT yaunda Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini Mradi wa HEET
Habari

OUT yaunda Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini Mradi wa HEET

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimeunda Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini  itakayosimamia na kufuatilia tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), chuoni hapo.
Katika uzinduzi huo, Mratibu Msaidizi wa Kitaifa wa Mradi wa HEET, Dkt. Evaristo Mtitu amesema kamati hiyo itatakiwa  kuandaa ripoti zote zinazohusiana na utekelezaji wa mradi huo.
Amesema ripoti hizo ndizo zitakazokaguliwa na mamlaka mbalimbali zilizoidhinishwa kufanya hivyo pamoja na wafadhili wa mradi ambao ni Benki ya Dunia.
“Huu ni mradi wa kimkakati hivyo malengo mliyojiwekea ambayo yalikubaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Dunia mnatakiwa kuyaangalia yatimizwe kwa uadilifu, Kamati hii ni jicho la utekelezaji wa huu mradi, hii ni dhamana kubwa sana mliyopewa,” amesema.
Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Elifas Bisanda, amesema kamati hiyo ni muhimu katika kipindi hiki OUT kinafanya utekelezaji wa Mradi wa HEET  katika kipindi ambacho ujenzi wa majengo ya maabara unaanza kwenye kanda saba.
“Huu mradi ni wetu, tumekuwa tukipata changamoto na gharama kubwa tunapofika kwenye suala la matumizi ya maabara,
“Mradi wa HEET unakwenda kutatua tatizo hilo hivyo kamati hii ikasimame vyema na imara kuhakikisha hakuna kinachoharibika kwa namna yoyote ile kwa kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa kufuata matakwa ya mradi,” amesema.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Tafiti na Huduma za Kitaalam na Mratibu wa Mradi wa HEET chuoni, Profesa Alex Makulilo, amesema baada ya uzinduzi huo,  kamati itahakikisha usimamizi na ufuatiliaji wa mradi unaimarika.
HEET unatekelezwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia udhamini wa Benki ya Dunia unaolenga kuimarisha taasisi za elimu ya juu katika maeneo ya miundombinu, ufundishaji na ujifunzaji ambapo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimepata takribani Dola Milioni tisa.

You Might Also Like

Silinde Akabidhi Nyaraka za Kufungua Masoko Mapya Nje ya Nchi

Rais Samia kufungua mkutano wa Mawaziri wa Uvuvi

Mkakati Wa Utekelezaji Wa Sera Ya Malikale Lango La Fursa Za Utalii

Midea Group Yafungua Duka Mlimani City Dar Es Salaam

TPHPA ina mchango mkubwa utoshelevu wa chakula – Profesa Ndunguru

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TARI Yawapa Elimu Wakulima, Maofisa Ugani 165 Kilimo Cha Matunda
Next Article Maboresho sheria, kanuni za madini yameongeza mapato
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?