MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Jeshi la Uhifadhi watakiwa kuzingatia mafunzo – Wakulyamba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Jeshi la Uhifadhi watakiwa kuzingatia mafunzo – Wakulyamba
Habari

Jeshi la Uhifadhi watakiwa kuzingatia mafunzo – Wakulyamba

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu

ASKARI wa Jeshi la Uhifadhi nchini wametakiwa kuyaishi mafunzo waliyopatiwa kwa lengo moja kubwa la kuipeleka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika viwango vya juu kiuhifadhi na kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya Uongozi kwa maofisa 159 na Askari Viongozi 77 katika Chuo cha Pasiansi Fort Ikoma, Serengeti

Wakulyamba amefafanua kuwa kupandishwa vyeo kwa askari hao ni matokeo chanya ya mapenzi makubwa ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Uhifadhi ili kuliimarisha liweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na Sheria za nchi kwa maslahi mapana ya Uhifadhi wa Maliasili zilizopo.

“Mafunzo haya ni muhimu sana, hivyo niwahimize kuyazingatia yote mliyofundishwa kwa kipindi chote mlipokuwa hapa chuoni. Mkafanye kazi kwa lengo moja kubwa la kuipeleka TANAPA katika viwango vya juu kiuhifadhi na kiuchumi” Akisisitiza Wakulyamba.

Wakulyamba amewasisitiza wahitimu wote kuepukana na kujihusisha na vitendo visivyofaa kwenye uhifadhi ikiwemo vitendo vya rushwa na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima wakati wa kutekeleza majukumu yenu ya kila siku.

“Ni jukumu lenu pia kujenga umoja na ushirikiano na askari pamoja na maafisa na kuondoa migawanyiko katika kazi”. Alikazia Wakulyamba

Ameupongeza uongozi wa TANAPA kwa kutoa kipaumbele kwa Wanawake kujipatia mafunzo na upandaji wa vyeo, huku pia amewapongeza askari wote kwa kuhitimu mafunzo haya muhimu, amewapongeza pia wakufunzi kwa juhudi kubwa walizozifanya zilizofanywa na wakufunzi wa mafunzo haya.

“Natumaini mafunzo haya yamewaongezea maarifa, ufanisi na uwezo wa usimamizi wa rasilimali za Wanyamapori na Misitu ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa”. Wakulyamba aliongezea

Naye Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Maendeleo ya Biashara TANAPA Massana Mwishawa amefafanua kuwa Mafunzo hayo yaliyofundishwa kwa njia ya nadharia na vitendo yalijumuisha pia matumizi sahihi ya silaha, ulengaji shabaha, usomaji wa ramani, ujanja wa porini na uongozi wa kijeshi.

Pia wamejifunza maadili ya kijeshi, uraia, ugaidi, ujuzi wa uongozi na kazi za ofisi kwa vitendo, usalama wa mtandao, amri za kudumu za jeshi la uhifadhi, ugavi na usimamizi, ukakamavu, uzalendo na uadilifu.

You Might Also Like

Mpango Kazi Wa Kupambania Haki Za Wenye Ulemavu Kuzinduliwa

Maziwa Kukuza Uchumi Wa Wafugaji

Rais Samia Kushiriki Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Ethiopia

Rais Samia Awakumbuka Wazazi Wanaojifungua Watoto Njiti

Fikeni kwa wakati CMA, mtatuliwe migogoro ya kikazi – Massawe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia awasili China kushiriki mkutano wa FOCAC
Next Article Tanzania kujiimarisha zaidi kidiplomasia – Majaliwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?