Na Lucy Lyatuu
CHAMA Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kimeshauri kuharakishwa kwa mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashauri kwa njia ya mtandao ( OCMS) kwa watumishi wa umma wa serikali kuu jambo litakalowezesha haki kupatikana Kwa wakati.
Kaimu Katibu Mkuu wa TRAWU,Edo Makata amesema hayo Dar es Salaam wakati akitoa maoni katika mfumo wa OCMS unaoratibiwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi(CMA) wa kuangalia masuala ya usuluhishi na upatanishi Kwa wafanyakazi.
Amesema mfumo huo Kwa CMA umekuja kwa wakati muafaka ambao nchi Iko Kwenye mpito wa migogoro ya wafanyakazi mahali pa Kazi katika suala zima la kuhakikisha haki inapatikana.
” Ni mfumo unaoweza kusaidia watu wengi ambao wanapata migogoro mahali walipo na kuepuka gharama za kufika CMA Kwa wakati asiokuwa na fedha,” amesema.
Amesema pamoja na manufaa yake lakini eneo la Tume ya Utumishi wa Umma linalohusikana na sheria za kazi za Umma lisiachwe.
Amesema mfumo wa OCMS umegusa sana sekta binafsi kwani ndio zinaangukia katika Tume ya CMA lakini watumishi wa umma kwemye vyama vya wafanyakazi kupitia ShirikishonlanVyama vya Wafanyakazi (TUCTA) wengi wao wako Serikali kuu.
Amesema kundi hilo linaangukia kwemye Tume ya Utumishi wa Umma ambao wanatumia Sheria za Utumishi wa Umma ambazo zina utofauti wake pia zenyewe mfumo huo uende kule kwa sababu kuna shida namna ya utoaji haki.
“Katika hali ya kuharakisha na kuifanya nchi iwe ni yenye kutoa haki kwa wakati suala hilo lizingatiwe,” amesema.
Ameongeza kuwa zipo kesi zinazokwenda hadi miaka 31 wakati huohuo mlalamikaji aliifungua akiwa na miaka 40 na kesi inapokwenda kwa miaka yote hiyo hufikia wakati mlalamikaji akiwa amefikia umri wa kustaafu na pengine kuondoka na hata kuingia umri wa uzee akiwa hajapata au kunyimwa haki yake.
Alitoa pongezi kwa CMA kwa hatuabwaliyofikia na kutaka elimu zaidi kuhusu mfumo huo iende Kwa wadau.