Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: HUDUMA za Mahakama ya Mwanzo kwa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, zinaanza kutolewa leo Agosti 12, 2024 katika Kituo cha Mahakama ya Mwanzo Kwembe.
Taarifa iliyotolewa na Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu – Kanda ya Dar es Salaam imeeleza kuhusu kuanza kutolewa kwa Huduma za Mahakama ya Mwanzo Kwembe katika Kituo cha Kwembe Wilaya ya Ubungo.
Taarifa hiyo imesema, Kituo hicho kinapatikana katika Jengo la Mahakama ya Wilaya Ubungo , Eneo la Luguruni Kata ya Kwembe, nyuma ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.