CHAMA cha Mabaharia Tanzania (TASU), kinaiomba serikali inunue au kutengeneza meli hata moja kwa ajili ya mizigo nje ya nchi na kuileta Tanzania ili vijana wanaomaliza vyuo wapate ajira.
Kaimu Katibu Mkuu wa TASU, Hamis Urembo amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa Mfanyakazi.
Urembo ameomba ombi hilo kwa kuwa hivi sasa ajira za mabaharia zimekuwa chache, ilhal chuo cha bahari kikiwa kinazalisha wanafunzi wengi kila mwaka ambao wanazagaa mitaani kwa kuwa hakuna meli za kuwasaidia.
“Sasa hivi tuna kiwanda kinatengeneza meli. Itengenezwe meli au inunuliwe nje ya nchi.
“Hapo zamani tulikuwa na kampuni ya ushirikiano ya meli ya China na Tanzania. Tulikuwa na meli nyingi kama MV Ruaha, MV Urafiki,
“Kupitia chama cha mabaharia kila baada ya miezi sita tulikuwa tunachukua mabaharia kwetu sisi, wanakwenda China, wanafanya kazi miezi sita, baada ya miezi sita wanapokezana, sisi tunafanya kazi kwa mkataba,” amesema.