Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 16

TPHPA Yatahadharisha Wakulima Kutumia Viuatilifu Kwa Njia Sahihi Kuepuka Madhara

Na Lucy Lyatuu,Tanga

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) imeendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu  na kushauri kuwa wanawake wakulima wasitumie viuatilifu kutokana na athari zinazoweza kufika hadi kwa mtoto.

Hayo yamesemwa na Mapulish  Hebel kutoka Kitengo cha Teknolojia za Vinyunyizi vya Viuatilifu cha TPHPA wakati akizungumza na wakulima wa mbogamboga mkoani Tanga katika maadhimisho ya siku chakula duniani yanayofanyika kayika viwanja vya Usagada.
Habari Picha 14141
Habari Picha 14142
Amesema haishauriwi wanawake kutumia viuatilifu kwa kuwa iwapo ataathirika upo uwezekano wa kumuathiri mtoto ambaye hajazaliwa ambapo mtoto atakuwa na shida hata kabla ya kuzaliwa.
Amesema pia wakati wa kunyonyesha  mtoto anaweza kupata shida na kutahadharisha kuwa makini na athari za viuatilifu kwa.matumizi yasiyo sahihi kwani yana uwezekano wa kuathiri ogani za ndani kama figo na ini.
“Mwanamke usijiangalie kuwa huzai au umemaliza bali tambua matumizi sahihi na kwa wakati sahihi,”amesema na kuongeza kuwa zipo namna mbalimbali za kumsaidia aliyeathirika  na matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu.
Habari Picha 14143
Habari Picha 14144
Kuhusu namna ya kumsaidia aliyeathirika na viuatilifu  alisema  jambo la kwanza mkulima anapaswa kuangalia  kibandiko kinasemaje namkujua iwapo kiuatalifu kimeingia mwilini kwa njia gani iwapo ni mdomo,pua ama kwa njia ya ngozi.
“Huduma ya kwanza kwa mhusika asitapishwe wala kupewa.maziwa kwankuwa viuatalifu vyenye asili ya mafuta hukimbilia kwenye sehemu yenye mafuta mwilini hivyo inashauriwa kukoroga unga wa mkaa  kijiko kimoja cha kula na kuchanganya na maji kisha kunywa,” amesema.
Habari Picha 14145
Habari Picha 14146
Habari Picha 14147
Amesema  pia mhusika anaweza kupewa mafuta ya nazi kwa kunywa katika maji ya moto,kutumia vitunguu swaumu ama kunywa ute mweupe wa yai.
Kwa upande wake Ofisa Kilimo wa TPHA, Saumu Mwesango amesema Mamlaka hiyo imekutana  na wakulima kupeana uzoefu wa  namna ya kutambua wadudu na wagonjwa kwenye mazao yao hasa ya mbogamboga.
Kadhalika alisema TPHA inawafundisha wakulima kujua teknolojia mbalimbali za mabomba namna ya kuyatumia,sifa zake,kiuatilifu anachotakiwa kutumia kulingana na aina ya wadudu ama magonjwa ta mimea.
i
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.