Na Lucy Lyatuu,Dodoma
MAMLAKA Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi Stad (VETA) imesema imeendelea kuboresha mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira, kupanua mifumo na fursa za mafunzo, kuimarisha mafunzo mahali pa kazi na kufanya tathmini ya mahitaji ya ujuzi
Tayari imeandaa mitaala mipya 29, wamefanyia mapitio mitaala 91, na kuboresha mitaala 13 ili iendane na Mfumo wa Mafunzo kwa Uanagenzi Pacha na programu ya Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya Shughuli za Uchimbaji Madini.
Kadhalika imesema katika kipindi cha 2022/2023 hadi 2025/2026, jumla ya waombaji 794 wa kujiunga na elimu na mafunzo ya ufundi stadi walikuwa ni wahitimu wenye elimu za ngazi za cheti, stashahada, shahada na hata shahada za uzamili.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore amesema hayo kagika mkutano na waandishi wa habari akielezea kuhusu Mamlaka hiyo na jukumu la kujenga Taifa la wananchi wenye ujuzi.

Amesema kuendelea kukua kwa uhitaji wa mafunzo kwa watu wenye elimu za juu
Uelewa wa umma kuhusu thamani ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi unazidi kukua, huku dhana ya ufundi stadi kuwa ni kwa ajili ya kundi fulani lililokosa fursa zingine za kielimu ukizidi kupungua.
Amesema kati wahitimu hao 522 walikuwa ni wenye vyeti vya taaluma zingine 120 walikuwa wenye stashahada (diploma),151 walikuwa na shahada na mmoja alikuwa ni mwenye shahada ya uzamili.
Aidha amesema kupitia programu ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo, katika kipindi cha 2022/2023 hadi 2025/2026, jumla ya mafundi 426 wenye elimu za juu waliomba kurasimishiwa ujuzi wao.
Amesema kati yao 82 ni wenye vyeti vya taaluma zingine 167 ni wenye stashahada, 170 ni wenye shahada na saba ni wenye shahada za uzamili .
“Unaweza kuona ni kwa namna gani jinsi watu wanavyotambua na kuthamini ufundi stadi, dhamira yetu ni kwenda mbali zaidi… tunatambua kuwa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanapaswa kupatikana kwa watu wote, bila kujali jinsia, mahali wanapotoka au changamoto wanazokabiliana nazo”, amesema Kasore.

Amesema Mamlaka hiyo imeweza kuongeza udahili wa wanachuo kwa mwaka katika vyuo vinavyomilikiwa na VETA kwa kiwango kikubwa, kutoka wanachuo 69,347 mwaka 2022/2023 na kufikia wanachuo 116,468 mwaka 2025/2026.
Vilevile, amesema VETA imeendelea kuwekeza katika utafiti, ubunifu na matumizi ya teknolojia zinazochochea uzalishaji na kutatua changamoto halisi za jamii.
Kasore amesema hadi kufikia mwaka wa fedha 2025/2026, bunifu 17 zilizotokana na elimu na mafunzo ya ufundi stadi zilikuwa zimefikia hatua mbalimbali za ubiasharishaji, huku bunifu zaidi ya 120 zikiwa zimeratibiwa na kuoneshwa katika maonesho na majukwaa mbalimbali.
Amesema miongoni mwa bunifu hizo ni simu ya VETA inayojulikana kama UjuziPro (Simu ya VETA), kifaa cha kuvunia matunda cha Lugobu, mashine mbalimbali za kilimo, Bajaji Road Sweeper Machine, pamoja na Smart Farming System, unaotumia Akili Unde (AI) kufuatilia na kusimamia shughuli za uzalishaji shambani.
Aidha, amesema VETA imeanzisha mfumo mfumo wa Fundi Connect ambao unasaidia kutangaza bidhaa za ubunifu na kazi za mafundi ili kuwapatia fursa zaidi za kibiashara.
Amesema katika kipindi kijacho, VETA imeandaa mtaala unaowezesha usimamizi wa taka ambaonutatoa mafunzo kwa wakusanyaji na wanaohifadhi kjjua namna ya kuzitunza.
” Mbali ya kukusanya taka hizo tutawapa ujuzi ilinkuona namna ya kuongeza thamani kwa taka hizo na kuwaingizia kkpato,” amesema Kasore.


