Na Lucy Lyatuu,Tanga
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Wametumia maadhimisho ya elimu,jjuzi na ubunifu 2026 kuelimisha umuhimu wa usajili wa Hataza (Patent), Alama za Biashara na Huduma, pamoja na namna wabunifu wanavyoweza kulinda kazi na bunifu zao.
Elimu hiyomimetolewa kwa maofisa wa BRELA kutembelea mabanda ya elimu na wafanyabiashara na wabunifu kuhusu hatua za kufuata ili kusajili bunifu zao na kupata ulinzi wa kisheria.
Katika zoezi hilo ,baadhi ya wafanyabiashara walipata fursa ya kusajili bunifu zao papo hapo na kuanza mchakato wa kupata hati zao za usajili.

Elimu hiyo pia ililenga kuwahamasisha wabunifu kuhakikisha wanasajili bunifu zao mapema ili kulinda kazi zao dhidi ya matumizi au kuchukuliwa na mtu mwingine bila ruhusa.
BRELA imeendelea kuhimiza wafanyabiashara na wabunifu kutambua thamani ya ubunifu wao na kuchukua hatua za kuusajili na kuulinda, kwani usajili si tu unatambulisha umiliki, bali pia unasaidia kulinda haki za mbunifu na kuongeza thamani ya biashara yake.



